Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 308
- 424
Tanzania imeweka historia kwa kuwa na Rais wa kwanza mwanamke, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Lakini pamoja na mafanikio makubwa aliyoyapata katika kipindi kifupi cha uongozi wake, bado anakabiliana na changamoto kubwa moja: mtazamo wa kijamii wa Kiafrika kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi. Jamii nyingi za Kiafrika zimejengeka katika mfumo dume unaoamini kwamba mwanaume ndiye mwenye haki ya kuongoza na kufanya maamuzi makubwa.
Hapa nitakupa uchambuzi wa kina ni kwa namna gani uongozi wake unavyoathiriwa na mitazamo ya kidini na mila na desturi zetu kama waafrika.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya kijamii ya uongozi barani Afrika (Afrobarometer, 2023) unaonesha kuwa kati ya Watanzania walioulizwa, sehemu kubwa ya waliokuwa na mtazamo hasi hawakuwa na sababu ya moja kwa moja ya kiuongozi, bali walihusisha jinsia yake kama kikwazo. Hii inaonesha kuwa tatizo si Samia kama kiongozi, bali ni jamii yetu yenyewe.
Mfano mdogo tunaupata katika dini ya Kiislamu. Wakati wanawake wanaposwali, imamu wao hakai mbele kama wanaume, bali hukaa mstari mmoja na wenzake. Hii ni hekima ya kidini yenye mizizi katika uelewa kwamba uongozi wa mwanamke kwa mwanamke mara nyingi ni changamoto kubwa. Ingawa hii ni mada pana inayohitaji mjadala wa siku nyingine, inaonesha tu mizizi ya changamoto ambazo hata viongozi wa kike kama Rais Samia hukutana nazo.
Pamoja na changamoto hizi, ukweli unabaki pale pale: Rais Samia ni kiongozi mzuri. Serikali yake imeleta mageuzi makubwa. Katika kilimo, ameongeza ruzuku za pembejeo, kuimarisha sekta ya umwagiliaji, na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. Katika elimu, shule mpya zimejengwa, madarasa yameongezwa na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka kutoka bilioni 464 mwaka 2020 hadi zaidi ya bilioni 780 mwaka 2024.
Sekta ya afya imepata msukumo mkubwa mno, vituo vya afya vimeongezeka, hospitali mpya zimejengwa na huduma za dawa sasa zinapatikana kwa zaidi ya 89% ya mahitaji. Miundombinu ya barabara imepanuliwa, mtandao wa barabara za lami umeongezeka kutoka km 13,235 mwaka 2020 hadi zaidi ya km 15,000 mwaka 2024. Sekta ya nishati nayo imeongezeka uzalishaji wake kutoka MW 1,602 hadi MW 3,078. Haya yote ni ushahidi wa uongozi makini wa Rais Samia.
Ni kweli mitazamo ya kijamii na dini huathiri namna wananchi wanavyomwangalia Rais Samia. Lakini bado, kila anapokwenda kwenye mikutano ya hadhara, maelfu ya wananchi hujitokeza kwa wingi kumshangilia. Hii ni kwa sababu matendo yake yanagusa maisha yao moja kwa moja. Watu wanapenda anachofanya, japo mara nyingine hofu zao za kitamaduni huwazuia kumkubali kwa moyo wote.
Kuhusu Chama cha Mapinduzi, hapana shaka chama hiki kimezidi kupendwa. Ushahidi wa picha na video kutoka mikutano ya hadhara unaonesha mapenzi makubwa ya wananchi kwa CCM. Rais Samia, kupitia kazi zake, amekifanya chama kionekane imara zaidi, kinachoelewa matatizo ya wananchi na kuyafanyia kazi kwa vitendo.
Changamoto kubwa inayomkabili Rais Samia Suluhu Hassan haiko kwenye sera zake wala maamuzi yake ya kiuongozi, bali imo katika mtazamo wa kijamii wa Kiafrika kuhusu nafasi ya mwanamke. Hii ni changamoto inayopaswa kushughulikiwa kupitia elimu, mabadiliko ya fikra na kuondoa vikwazo vya kitamaduni.
Hata hivyo, kwa kazi kubwa alizofanya kwenye kilimo, afya, elimu, miundombinu na sekta nyingi, historia itamkumbuka kama kiongozi aliyeliletea taifa maendeleo, licha ya mitazamo ya kijamii iliyompinga kwa sababu ya jinsia yake.
Hapa nitakupa uchambuzi wa kina ni kwa namna gani uongozi wake unavyoathiriwa na mitazamo ya kidini na mila na desturi zetu kama waafrika.
Mila, dini na mtazamo wa kijinsia
Ukweli ni kwamba, sehemu kubwa ya changamoto anayozokutana nazo Rais Samia zinatokana na jinsi jamii zetu zilivyojengeka. Mila nyingi bado haziko tayari kumpa mwanamke nafasi ya juu ya uongozi. Dini na desturi zetu zimekuwa zikihalalisha imani hizi. Kwa mfano, tafiti kadhaa za kijamii zinaonyesha wazi kuwa bado kuna idadi kubwa ya watu ambao hawampendi Rais Samia si kwa sababu ya uongozi wake, bali kwa sababu tu yeye ni mwanamke.Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya kijamii ya uongozi barani Afrika (Afrobarometer, 2023) unaonesha kuwa kati ya Watanzania walioulizwa, sehemu kubwa ya waliokuwa na mtazamo hasi hawakuwa na sababu ya moja kwa moja ya kiuongozi, bali walihusisha jinsia yake kama kikwazo. Hii inaonesha kuwa tatizo si Samia kama kiongozi, bali ni jamii yetu yenyewe.
Ulinganisho na mataifa ya Ulaya
Kama tukigeukia mataifa ya Ulaya, hali ni tofauti kabisa. Wanawake wamepewa nafasi kubwa ya kuongoza bila upinzani wa kijinsia. Angela Merkel wa Ujerumani aliongoza taifa lake kwa zaidi ya muongo mmoja na aliheshimika dunia nzima, si kwa sababu ni mwanamke, bali kwa sababu ya matokeo ya kazi yake. Katika nchi nyingi za Ulaya, jinsia si kikwazo cha kupimwa uwezo wa mtu. Kwa Afrika, bado ni kizungumkuti na tuna safari ndefu sana.Changamoto ya wanawake kwa wanawake
Kisaikolojia, mwanamke mara nyingi anakuwa tayari zaidi kumpa heshima mwanaume kuliko mwanamke mwenzake. Katika familia, katika jamii na hata katika taasisi, wanaume hupewa heshima ya kiasili. Kwa wanawake, uongozi wao mara nyingi huamsha mashaka kwa wenzao wa kike. Ndiyo maana ni rahisi zaidi mwanamke kupoteza ushawishi miongoni mwa wanawake wenzake.Mfano mdogo tunaupata katika dini ya Kiislamu. Wakati wanawake wanaposwali, imamu wao hakai mbele kama wanaume, bali hukaa mstari mmoja na wenzake. Hii ni hekima ya kidini yenye mizizi katika uelewa kwamba uongozi wa mwanamke kwa mwanamke mara nyingi ni changamoto kubwa. Ingawa hii ni mada pana inayohitaji mjadala wa siku nyingine, inaonesha tu mizizi ya changamoto ambazo hata viongozi wa kike kama Rais Samia hukutana nazo.