Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,668
- 149,840
Ninaamini tungekuwa na waandishi wanaowabana vizuri viongozi kwa maswali bila kuwaogopa au kuwaonea aibu, press conference hizi za kila wakati hakika zisingekuwepo na badala yake wangekuwa wanatoa press release tu.
Kwa mfano, kiongozi anaweza kuwa ametoa ahadi fulani lakini kabla hajaitimiza ndani ya muda aliopanga akaibuka na jambo jingine na kuita waandishi ambao nao wanaweza hata wasimuhoji kuhusu utekelezaji wa ahadi zake za awali na wakabaki tu kushabikia tukio jipya wakati yaliyopita hayajakamilika kama alivyoahidi.
Leo hii sitashangaa waandishi wakaitwa na kupewa taarifa ya bomoabomoa pasipo wao kuhoji hatima ya baadhi ya majengo nyeti ambayo mpaka sasa serikali iko kimya licha ya majengo hayo nayo kutajwa kuwapo katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Halikadhalika,sitashangaa siku waandishi wakaitwa na kupewa taarifa za waliosafiri bila vibali na hatua walizochukuliwa na wasihojo ya CAG.
Hata wakati Baraza la Mawaziri linatangazwa na hata hivi juzi Makatibu Wakuu walipotangazwa sidhani kama waandishi waliohoji ni kwanini baadhi ya watu wenye tuhuma fulani fulani wamepewa tena nafasi katika hii serikali tunayoambiwa imekududia kuleta mabadiliko.
Mpaka leo hii sidhani kama kuna mwandishi aliedhubutu kumuhoji Raisi au Katibu Mkuu Kiongozi kutaka kujua msimamo wao kuhusu zoezi zima la uuzwaji wa nyumba za serikali na hatua gani zitachukuliwa iwapo kuna nyumba ziliuzwa kinyemela na hata kumuhoji raisi mwenyewe iwapo zoezi lile lilikuwa sahihi.
Mpaka leo hii sidhani kama kuna mwandishi aliethubutu kuhoji fedha za elimu bure ziliizipitishwa na Bunge gani au hata kutaka kujua utaratibu uliotumika kuidhinisha matumizi ya fedha hizo.
Mpaka leo hii sidhani kama kuna mwandishi aliefuatilia na kujua kama kweli yule mgonjwa wa Muhimbili matibabu yake yaligharamiwa na Raisi kama alivyoahidi au laa na sidhani kama kuna mwandishi atakaethubutu kumuhoji Raisi juu ya hilo siku wakialikwa Ikulu au pale nafasi ya kuongea na raisi itapojitokeza.
Inashangaza mpaka sasa waandishi wanashindwa kumuhioji Raisi au Katibh Mkuu Kiongozi ni kwanini mpaka sasa hakuna mwanasiasa hata mmoja aliewajibika zaidi ya watendaji wakuu wa mashirika na Taasisi za umma na badala yake wengine wanahoji kupitia media zao wakati walikuwa na fursa ya kuwahoji viongozi wahusika ana kwa ana.
Yako mengi na hii ndio sababu ya bwana wakubwa hawa kutohofia kuita waandishi kila wakati.

Last edited by a moderator: