Mtazamo:- Dar itaendelea kuwa ya mwisho kielimu

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,754
7,091
Nadeclare interest kuwa Mimi ni mdau na mshirika wa Elimu.
Najikita wilaya ya kinondoni nilipofanyia utafiti wangu na kubaini yafuatayo:-

1: Wanafunzi wa shule ya msingi kurejeshwa nyumbani SAA nane pale ratiba ya shule inapogota.

2: Walimu kupigwa marufuku kuendesha remedial shuleni na nje ya shule. Ushahidi ni waraka uliotiwa saini na mkurugenzi wa manispaa.

3: Ziara za mkuu wa wilaya kuhamasisha Elimu bure na kupiga marufuku masomo ya ziada mashuleni na nje ya shule za umma.

Hii kiuhalisia itaufanya mkoa na hasa wilaya zake kuwa na matokeo machafu kuliko yale ya mtwara kwani mtoto wa age ya under 14 years kumwacha ajiongoze peke yake bila uangalizi wowote tangu saa nane hadi wazazi warudi usiku kutoka vibaruani ni kutokuwatendea haki watoto wenyewe na wazazi wao.

Pia kuwanyima walimu kutumia muda wao wa baada ya kazi kuwafundisha watoto watakaohitaji eti watawaoendelea hadi madarasanu haina mashiko.
Hapa namaanisha kuwa suala LA kumpangia mwalimu kwenda kulala Mara baada ya kazi yaani kuanzia SAA 9.30 jioni huku viongozi mnalia juu ya kushuka kwa uchumi na kuwaacha baadhi ya wafanyakazi wengine kufanya part time Kama madaktari na manesi ni kuonyesha jinsi mnavyozidi kuwa maadui wa walimu.

Ni kwanini mkuu wa wilaya badala ya kutafuta mbinu za kuwafanya watoto wabaki maeneo ya shule hadi saa 11 jioni yeye anawakataza walimu kufanya Nazi hiyo.

Msisahau mwalimu huyu mnayemwandama kwa kila hali naye Ana akili zake.
Nashauri yafuatayo kwa wizara husika:

Ihusike kutoa miongozo kwa walimu na sio itoke kwa wakurugenzi.
Waingilie kati hili la kumkataza mwalimu kufundisha nje ya eneo la shule baada ya saa za kazi kwani muda huo ni wake na sio wa mwajiri na watoto hao in wa wazazi na sio wa umma kwa muda huo.

Mkuu wa wilaya na mkoa kaeni na walimu mtafute suluhu ya shule zenu kushika mkia kitaifa na sio kuwabania walimu.

Isije kuwa suala hili in LA kisiasa hivyo tuakomoana badala ya kujengana. Tukumbuke siku zote matokeo ya mwisho ya mwanafunzi mtu wa kufurahi au kuumia ni mzazi na sio mkuu wa wilaya. Wazazi mnasemaje juu ya hili?
 
Kama ni kweli na kiongozi wa mkoa kafoji vyeti ndo kabisaa watoto hawatajali kujibidisha na masomo.Waumize vichwa kwa nini wakati wanaweza nunua vyeti huko mikoani na wakawa viongozi ! Kazi ipo.
 
Back
Top Bottom