kamati ya ufundi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 416
- 439
USAHIHI HUU HAPA!!
MTATIRO NA HOJA YA RUZUKU NI UZUSHI KAMA HOJA YA RITA .
CUF Chama cha Wananchi kinawataka Wang achama wake kupuuza propaganda inayosambazwa na Genge la Cufchadema kwamba wameshinda Kesi ya Madai ya Ruzuku leo hii katika Mahakama Kuu.
Kimsingi Maalim Seif na Vijana wake ni watu wanaoishi kwa Matumaini ndani ya Chama cha CUF, ni kweli walipeleka Ombi la kutaka kumshitaki Msajili wa Vyama, huku dai lao Kuu likiwa ni Tshs 369 million zilizoingiwa kwenye akaunti ya Chama iliopo NMB Temeke shauri hilo namba 21 /2017 limetajwa mara mbili tu na bado inaendelea kusikilizwa mbele ya Jaji Dyansobera. Katika shauri hilo, waombaji waliweka Ombi dogo la kutaka Mahakama wakati inaendelea kusikiliza Kesi ya msingi, imzuie Msajili asitoe Ruzuku upande wowote ule katika pande hizi mbili zinazovutana.
Kesi hiyo imesikilizwa leo bila ya kuwepo upande wa Walalamikiwa yani Msajili wa Vyama na Mwanasheria Mkuu na Wakili wa upande wa Walalamikaji walijenga hoja pekee yao na Kisha Jaji akawapa ruhusa ya kumfungulia Kesi Mwanasheria Mkuu na Msajili wa Vyama kama walivyoomba na pia amekubali kwa kipindi hiki ambapo Kesi ya msingi itakua inasikilizwa basi pasitolewe Ruzuku kwa upande wowote ule.
Sasa huku si kushinda Kesi bali ni kushinda Ombi dogo katika Kesi ya Msingi.
Tatizo Kubwa kwa wenzetu ni kufanya kila kitu kua propaganda, kwenye hili wenzetu wanarudia jambo lile walilofanya Juzi kuhusu suala la Rita.
Utashindaje Kesi ambayo hata haijaanza kusikilizwa?
Sio kila kitu kiwe Propaganda, tunawatoa khof Wanacuf msiwe na mashaka achaneni na hoja zakujipa Matumaini zinazofanywa na Cufchadema.
Chama Cha CUF kipo imara na kinaendelea kuwepo
Abdul Kambaya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Cuf Taifa