Mtanzania Koku Gonza ndani ya Empire TV Series

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Ile TV series inajulikanayo kama Empire Katika msimu huu ambao ni msimu wake wa 3 hatimae Mtanzania ambaye pia ni muimbaji aishiye Marekani katika jiji la Chicago dada yetu Kokugonza ameshiriki.

KOKU.jpg

Koku anaonekana kwenye scene moja akimfundisha Hakeem kucheza piano. Na ijulikane kwamba Koku Gonza anakipaji cha kucheza Piano pia.

12472352_10205490705336479_2705412072019449767_n-200x200.jpg

Koku Gonza akiwa na muigizaji mwenzie Hakeem.

Sema mumarekani mwenye asili ya kitanzania,sio mtanzania.kwani tanzania hamna sheria ya kuwana uraia wa nchi 2

Pia empire ya season ya 3 ilikwisha na huyo bi mdada hakuwepo.itakuwa empire ya msimu wa 4
 
Huyu ni Mhaya aliyeamua kutenganisha majina yake yaonekane kama jins lake koko na la babayake gonza, kumbe ni KOKUGONZA ikiwa ina maana kwamba upendo
;hahaha ina maana Nakupenda..Bigonzo ina maana ya MAPENZI... muhaya halisi huyo
 
Ile TV series inajulikanayo kama Empire Katika msimu huu ambao ni msimu wake wa 3 hatimae Mtanzania ambaye pia ni muimbaji aishiye Marekani katika jiji la Chicago dada yetu Kokugonza ameshiriki.

View attachment 335179

Koku anaonekana kwenye scene moja akimfundisha Hakeem kucheza piano. Na ijulikane kwamba Koku Gonza anakipaji cha kucheza Piano pia.

View attachment 335186
Koku Gonza akiwa na muigizaji mwenzie Hakeem.

wahaya katika ubora wao am proud to be the haya....
 
Sema mumarekani mwenye asili ya kitanzania,sio mtanzania.kwani tanzania hamna sheria ya kuwana uraia wa nchi 2

Pia empire ya season ya 3 ilikwisha na huyo bi mdada hakuwepo.itakuwa empire ya msimu wa 4
mhhh empire season 3 imeisha ? wakat hata season 2 bado haijaisha.
 
Sema mumarekani mwenye asili ya kitanzania,sio mtanzania.kwani tanzania hamna sheria ya kuwana uraia wa nchi 2

Pia empire ya season ya 3 ilikwisha na huyo bi mdada hakuwepo.itakuwa empire ya msimu wa 4
Mkuu utakuwa unahesabu session za kuoneshwa! Empire huwa inaanza late summer na inapofika winter, wanachukua break! Winter ikipita ( mwaka unakuwa umeshapinduka) wanaendelea walipoishia previous year for the same season. Kwahiyo bado tupo season 2!
 
Kokugonza ni Mtanzania, ni mtoto wa marehemu Longino(Longfellow) Mugarula wa Kiziba, Kashasha karibu kabisa na chuo cha ufundi kashasha.

Baba yake aliishi Marekani, mbali na kuwa msomi mbobezi (PhD holder) alikuwa pia mwanamuziki maarufu. Ameimba nyimbo nyingi sana kwa lugha mbalimbali na ameishi katika nchi mbalimbali km Finland, South Africa, canada n.k. Na kote huko aliiimba kwa lugha zote za wenyeji.

Kokugonza ni mjukuu wa Mzee Martine Mugarula, huyu alikuwa mmoja wa wasomi wa mwanzo kabisa wa sheria mkoani Kagera. Alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya awamu ya kwanza, alikuwa hakimu, ofisa wa polisi nk. Alifariki ghafla hospitali ya mkoa wa Kagera mwaka 1988.

Kokugonza ana dada zake wengine wawili ambao Longfellow aliwazaa hukohuko Marekani, wanaitwa Ntangilege na Tibeshara Mugarula.

Inapendeza baba yao aliwapa majina ya asili kutoka Bukoba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom