Mtanzania afungwa miaka 30 Kenya kwa kusafirisha madawa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mahakama ya Mombasa, Kenya imemhukumu Mtanzania Hussein Idd kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya Sh milioni 90 za Kenya (zaidi ya shilingi bilioni 2 za Tanzania) kwa kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Edgar Kagoni amemhukumu Mtanzania huyo aliyekutwa na hatia ya kukutwa na kilo 10 za heroine Machi mwaka jana kwenye hoteli ya Regency, Mombasa.

Hakimu Kagoni amesema, endapo Idd atashindwa kulipa shilingi milioni 90 za Kenya ataongezwa miaka mitano mingine jela.

Julai mwaka jana, mahakama hiyo ilimhukumu Mtanzania mwingine, Harun Bakari Juya kifungo cha miaka 20 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 26.6 za Kenya (zaidi ya sh milioni 603 za Tanzania).

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Juya alikamatwa alipofika Lungalunga Kenya akitoka Tanzania akiwa na kilo 2.975 za dawa za kulevya aina ya heroine zanye thamani ya sh milioni 8.9 za Kenya.
 
Mambo Kama haya ndio utasikia kitengo Cha passport wanasema ohhh tukupe ukienda kuuza madawa huko itakuweje.Wewe mpe mtu passport huko nchi za watu pia Kuna serikali,vyombo vya dola,mahakamani na jela.Muwaamini na nchi zingine pia.Si unaona huyo kadakwa sababu kule nako Kuna mifumo ya kushughulika wahalifu.Msiogope kumpa kila mtanzania passport kisa maruhuni wachache Kama huyu aliyedakwa Kenya.Huyu Ni tone Katika bahari ya watanzania wema milioni hamsini.Uhamiaji woga wa kutoa passport ondoeni.Hongereni Kenya kumdaka na kumpa hukumu.inayomstahili haaibishi watanzania anajiaibisha mwenyewe kila mtu abebe mzigo wake
 
Niendelee kumpongeza makonda kwa Kaanzisha Harakati hizi ukanda huu
Hongera sana pia Kenya kwa kua macho nina Hakika tukishirikiana tutamaliza tatizo hili
 
Hadi nimelegea maana Jina hili linatoka kufanana jina la rafiki yangu mmoja tumekuwa pamoja na tumesoma pamoja alibahatika kupata diploma ya ualimu kwa masomo ya fizikia hesabu na kemia na tayari alingia Kwenye Ajira shule moja pale Arusha lakin mda mwingi sana root zake alikuwa anaenda sana Kenya na sikujua ni biashara gani anafanya lakin pia alikuja kupotea ghafla mpaka leo na ndio nasikia hili Jina nimetetemeka had maini. NAJUA JF HUWA HAMTUANGUSHI KWELI HATUWEZI KUPATA HATA PICHA YAKE.
 
Mkuu huko Lumumba wameshindwa kabisa kukutafutia hapo hata invitation letter ili iwe rahisi kwako kuomba passport? Mana Hilo povu kwa uhamiaji sio mchezo.
 
Mkuu unataka waende mpelampela kwa maslahi yanani?
 
Aiseeee Edwin kumbe yupo toka 2011
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…