Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,500
- 9,279
Mahakama ya Mombasa, Kenya imemhukumu Mtanzania Hussein Idd kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya Sh milioni 90 za Kenya (zaidi ya shilingi bilioni 2 za Tanzania) kwa kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
Hakimu Mkazi Mwandamizi Edgar Kagoni amemhukumu Mtanzania huyo aliyekutwa na hatia ya kukutwa na kilo 10 za heroine Machi mwaka jana kwenye hoteli ya Regency, Mombasa.
Hakimu Kagoni amesema, endapo Idd atashindwa kulipa shilingi milioni 90 za Kenya ataongezwa miaka mitano mingine jela.
Julai mwaka jana, mahakama hiyo ilimhukumu Mtanzania mwingine, Harun Bakari Juya kifungo cha miaka 20 jela na kulipa faini ya shilingi milioni 26.6 za Kenya (zaidi ya sh milioni 603 za Tanzania).
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Juya alikamatwa alipofika Lungalunga Kenya akitoka Tanzania akiwa na kilo 2.975 za dawa za kulevya aina ya heroine zanye thamani ya sh milioni 8.9 za Kenya.