aminiusiamini
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,577
- 2,226
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa nafasi hii.
Tunapokwenda kwenye uchaguzi mkuu,ndugu zangu watanzania nawaomba sana tuachane na hii tabia ya kupakana matope na siasa maji taka.Tajaribu kuongea kwa lugha njema yenye kukubalika na kuheshimiana mawazo.
Kamwe hatuwezi kukubaliana katika kila jambo lakni tukubaliane katika kutunza amani ya nchi,utu na desturi zetu sisi watanzania.Naomba wale wanaopokea fedha kumtukana mgombea fulani kwa matusi na mambo mengi yasio faa naomba waache.Ushabiki hautatupeleka popote,zaidi ya kutuleta shida na magomvi ambapo hao tunaowashabikia wanakula kuku kwenye mahekalu yao sisi tukiishi kwa shida baada ya uchaguzi.
Tumwombe Mungu sana kwenye hili jambo.Tumchague mtu anayeweza kutuletea maendeleo na tuache matusi na lugha chafu.
ahsante