Niliwahi kumsikia Joseph Kusaga anasema yeye kwenye Ajira zake za Utangazaji huwa haangalii suala la Elimu anachokiangalia ni kipaji chako hata kama umeishi la Saba.
Naamini ndio ukweli wenyewe na wengi wameamua kufuata mtindo huo wa kuangalia vipaji zaidi na sio Elimu, ndio maana tunawasikia Wakina Mpoki, Zembwela, Gigy money japo sijui huyu waliangalia kigezo gani n.k
Wameona kwa wenzao wakenya na wao wanaangalia Kipaji zaidi kuliko elimu ndio maana Redio zao nyingi zimejaa wachekeshaji.
Ubaya wetu tumebaki kuwaangalia wale wale tu na hivyo tunakuwa kama tunawagombania badala ya kuibua hawa ambao wana elimu lakini pia wana kipaji ambao wamekosa watu wa kuwashika mkono.