Mtangazaji Masoud Masoud wa TBC

Huyu Mwamba huwa namsikia Jumamosi asubuhi. Aisee hana mpinzani kwenye narrations . Nilimsikia siku moja akisimulia ajali ya ndege ya wale wachezaji wA Zambia, Yani anakuchukua anakuweka ndani ya tukio. Ni muvi aisee! Najiuliza tu anawezaje juwa vitu vyote hivii!?? Je hawazi kuziweka hizi simulizi kwenye kitabu!? Alafu mbona hayupo kwenye social media!!?
 
Siku moja alikua ana muelezea whitney Huston...... Aisee jamaa alikwenda deep sana nikawa kama naangalia documentary kwente Tv kumbe nasikiliza redio

Kuna siku alikua anachambua aina za sauti na uwezo wa waimbaji duniani, hapo ndipo nilipo kuja kubaini kuwa Ruby anakipaji cha hali ya juu sana cha sauti miongoni mwa wanamuziki wa kibongo
 
Angekuwa anafanya freelancer anazunguka vyombo tofauti tofauti huko alipo sidhani kama anaonekana ipasavyo...

Ila ndio hivyo huenda ni maslahi huko Pengine if It don't make Dollars then it don't make Sense.....
 
Amefanya kazi redio kubwa karibu zote
 
Jamaa ana msimamo sana
 
Mwanamziki wa kweli kweli ni yule anaepiga hela for future ww na sauti yako nzur huna lolote umaarufu mjin PESA
Huo ni mtazamo hasi mkuu, kila mtu anahitaji pesa lakini wapo wanaoridhika mapema ingawa wangeamua wangezimake.
 
Yap...nilikisikia hicho kipindi...nafikiri haswa alikuwa anamzungumzia UMU KULUTHUUM wa Egypt
 
Mtangazaji kama huyu katika miaka ya sasa ni ngumu kumpata kama wapo basi ni wachache sana wa kuhesabu. Amewai kuchambua kwa kusema uu wapi Mziki wa Tanzania kwenye mizania ya kimataifa, tukisema tuonyeshe muziki wetu tutasema ni Bongo Fleva au Amapiano.. anasema chembe yenye asili ya muziki wa Tanzania ilibakia kwa Msondo na Sikinde na bado haoni wa kuuendeleza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…