Mtandao wa viber sasa wafuata nyayo za apple na whatsapp katika usalama

blogmaster

Senior Member
Aug 15, 2015
167
74
viber-700x325.png

Makampuni mengi yanayojihusisha na teknolojia siku hizi yanathamini ulinzi na usalama wa taarifa za wateja wake sana. Kwa mfano tumeona kampuni ya Apple ikipinga maamuzi ya FBI kutaka kufungua moja ya simu yake.

Pengine baada ya tukio hilo la iPhone ndio ndio limepelekea mtandao wa Whatsapp kuimarisha ulinzi wa mazungumzo baina ya mtu na mtu.

Njia hii ya ulinzi na usalama ina uwezo mkubwa wa kuzuia serikali, wadukuzi na watu wengine kuweza kupekua kwa siri taarifa zako za mazungumzo baina yako na mtu mwingine. Kumbuka awali ilikuwa ni rahisi kabia kujua watu wanazungumza nini katika mitandao yao ya kijamii kwa kuwa teknolojia hii ilikuwa haijaanza kutumika sana.

Kufuatia tukio hilo, Viber nao wamesema kuwa hawawezi kubaki nyuma katika teknolojia hii. Katika teknolojia hii kama ilivyo katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp. Huduma hii ya ulinzi na usalama itakuwezesha kutuma na kupokea mazungumzo ambayo yana ulinzi wa hali ya juu kabisa.

End-to-end Encryption inapatikana katika toleo la Viber namba 6.0. Kingine kizuri kuhusiana na teknolojia hii ni kwamba hata mtandao wenyewe utakuwa hauna uwezo wa kusoma meseji zako. Yani kwa mfano ukiwa unatumia teknolojia hii mitandao kama vile viber na Whatsapp itashindwa kusoma meseji zinazoenea kupitia mitandao yake.

Wakati unafanya mazungumzo na mtu utaona kimetokea kikufuli chekundu, ukiona hivyo tu basi ujue inamaanisha kwamba mazungumzo yenu yanalindwa.

Viber imesema toleo hili mpaka kufikia muda wa siku mbili litakuwa tayari linapatikana duniani kote. Viber ina watumiaji zaidi ya milioni 700 ambao wanatumia mtandao hu mara kwa mara. Na kwa maboresho haya namba hiyo inaweza ikapanda kwasababu watu wanapenda usalama.

Apple ndio ilikuwa kampuni ya kwanza kuja na teknolojia hii na ikafuatiwa na Whatsapp na sasa Viber ambapo inaonekana kabisa makampuni haya matatu yanajali sana taarifa za watumiaji wake
 
kwa hiyo mkuu sitaweza kutumi whatsapp ya mtu at the same time. i mean nikiinstal kwa sim yangu halaf nimchabo
maana hii trick naikubali san.
 
Back
Top Bottom