Dumelang
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 3,203
- 5,704
Habari wanajamii
Kumekuwa na Wimbi kubwa sana la utapeli dhidi ya wazee wastaafu hivi karibuni, wanatapeliwa fedha wanazopata mara wanapostaafu, wizi huu umekua sana katika siku za hivi karibuni
Naimani habari hizi wengi mnazijua na mmezisikia , tangu mwaka huu uanze nna habari tatu tofauti za wazee waliostaafu kudanganywa na kutapeliwa mafao yao yote pale tu wanapoyapokea.
Kwa jinsi inavyoonekana mtandao huu ni mpana na bila shaka kwa jinsi visa hivi vinavyotokea matapeli hawa huwa wanafanya kazi ya kujua au kutambua wastaafu na kuwafuatilia, kisha kuwaadaa na badae kuwaibia kwa njia za kitapeli.
Tukio la kwanza ni la mfanyakazi mwenzangu alie staafu mwaka jana na akadanganywa na kupigwa pesa yote mwaka huu mwanzoni .
Mwezi uliopita nilipata habari kama hii.
Leo asubuhi nimepata habari ya mstaafu mwingine alietapeliwa na kisha kunywa sumu (habari Ambazo azijathibitishwa) na yupo hospitali akiendelea na matibabu
Wimbi la utapeli kwa wastaafu linashika kasi sana, na bila shaka hii ni chain kubwa sana inayohusisha watu maalum ili kuwatambua wanaopokea mafao (wastaafu).
Ombi langu kwa serikali kwakuwa taarifa hizo zipo polisi huko, itafutwe namna ya kukomesha uhalifu huu na kuwalinda wazee wetu hawa.
Taasisi zinazotoa mafao zitoe elimu juu ya wizi huu wa kutapeliwa fedha hasa kwa wastaafu ambao ni wateja wao.
Jamii tuwalinde, tuwashauri, tuwe makini na nyendo za wastaafu ambao ni ndugu na jamaa zetu wanapokuwa katika harakati za kustaafu na kupata mafao.
Naomba kuwasilisha, imani yangu ni kuwa wadau mmeshaliona hili katika jamii huko.