Mtandao wa tume ya uchaguzi Ghana wadukuliwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_92883782_64e13576-81dd-4371-8f6f-b4b1e0c2431a.jpg

Wadukuzi wa mitandao wamevamia mtandao wa tume ya uchaguzi nchini Ghana na kuuvuruga siku moja baada ya uchaguzi wa urais katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

Tume ya uchaguzi nchini Ghana inasema kuwa imelaani jaribio hilo la kuudukua mtandao wake.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter tume hiyo ilisema kuwa taarifa inayodai kuwa mgombea wa upinzani Nana Akufo Addo alikuwa mbele ya rais wa sasa John Mahama ilikuwa ya uongo.

Haijabainika ikiwa taarifa hiyo ilionekana kwenye mtandao wa tume ya uchaguzi, ambao kwa sasa unaonekana kukumbwa na matatizo.

Chanzo: BBC
 
Hukumbuki walibebwa na kamanda kova kina mussa Allan Yeriko Nyerere Ocampo four walikuwa wanayadukuwa matokeo ya uchaguzi
 
Hukumbuki walibebwa na kamanda kova kina mussa Allan Yeriko Nyerere Ocampo four walikuwa wanayadukuwa matokeo ya uchaguzi
 
Sasa walikuwa wanajulisha kwa
Njia ipi kama siyo kuhack kwanza
Matokeo yanaanzia kwao wanayachakachua ndyo wanayatuma nec au unafikiri walikuwa wanayakusanya kwenye vituo?
 
Uwongo hawakudukua walikuwa wanajumlisha ndio maana mahakama imewaachilia huru!
Mahakama haikuwaachia bali Serikali kupitia waendesha mashtaka wake iliamua kutoendelea na kesi.

Nadhani Serikali iliwaonea huruma kwa kujua walikuwa wanatumika tu bila kujijua.
 
Back
Top Bottom