Mtandao wa LUKU Una tatizo gani?

Mtandao wa LUKU Una tatizo gani?

Nimejaribu kununua LUKU by crdb mobile naambiwa sina sali sijaelewa hapa jamani

Simu yako haina vocha, kila Meseji nadhan service provider kama voda wanachaji sh 50+
Tia vocha mkuu
Nb ...sio kifurushi, wanakula kwenye Salio la vocha
 
Mkuu kwenye benki waweza kuweka na KUTOA, kuweka hakuna sharti lolote isipokuwa KUTOA.
Hii ni kwa kuwa kuweka anaweza kuweka mtu yeyote na kutumia simu yoyote ila KUTOA lazima uende benki waisajili iyo laini ya simu. Sasa kama bila kujisajili wakiruhusu uamue mwenyewe sasa na jirani si ataamua mwenyewe ivo akatoa kwako ? Lazima ukajisajili mkuu

Hapana hujanielewa .......unaweza hata kuwa benki ukaambiwa system mbovu hadi kwenye ATM ......hivyo wanapokea tu pesa ila si kutoa .......nimewahi kudokezwa jinsi huu uhuni unavyofanywa na kusingizia system ........
 
OK kwenye ishu kama izo mm sijajua labda utupe uzoefu next time tujue way forward na sisi wengine.
Ila ATM ikifeli na ww ukiingia unaona, kumjua adui ni sehemu ya ushindi, tupe uzoefu mkuu!!
 
LWITIKO umefanikiwa? Ukiweka vocha nunua tena. Otherwise nasepa nawai sherehe za mapinduzi uku kwetu!
 
Ila angalizo wakuu, ukipewa bill ya umeme au luku jaribu kuhakiki, angalia unit cost times no.of units ongeza other charges kwa% walizotaja, nilipigwa mwezi nNovember nimefanya hesabu nkakuta matumizi ni madogo zaidi ya units nilizoconsume, nimeenda tanesco tukafanya hesabu wakasema kuna shida ivo nisilipe decemba na januari nzima, kuna kausanii wakuu, ALL IN ALL KUWA MAKINI.
 
Mkuu ni Mteja wa crdb?
Labda nkuelekeze nilivonunua?
Inakubali maybe nisijue kama ni network kwenye zone yako
Au tafuta wakala wa crdb

Nashkuru sana kwa Ushauri wako Mkuu, nmetumia Nmb Mobile na nmefanikiwa kupata units za Kutosha bila Zengwe...,
 
Kwani hujui Tanzania mvua ikinyesha kila kitu kinakuwa matatizo. Kuanzia mabomba kupasuka, vingamuzi ku kwama kwama, Barabara kujaa maji/maafuriko, umeme kuzimwa, na hata network zote kushindwa kufanya kazi kuanzia za simu hadi hizo za luku.
 
Kupanga ni kuchagua ...umeamua mwenyewe kukaa foleni.
Zifuatazo ni njia mbadala

1. Mpesa
Wewe kama ni Mteja wa mpesa, tigo zantel au airtel unakaa kitandani kwako unaingia kwenye menyu unanunua umeme unapewa TOKEN na kusimama, elekea kwenye mita yako tia umeme.
FOLENI UMEITAKA MKUU

2. CRDB BANK
wewe kama ni Mteja wa benki ya crdb kuna njia kuu2
i. Ingia menyu yao kwa *150*03# ingia kwenye Akaunti yako nunua umeme then unapata token ukiwa apo apo chumbani kwako.

ii. Tafuta wakala yeyote wa crdb mwambie hela hii apa nataka umeme ...ataingia kwenye machine yake na kukupatia risiti yenye token
Wakala wa hii benki nawaona kila mtaa, mtaani kwetu wapo wa3 ....
Office nyingi za posta ni wakala wa crdb.

Mwisho:
Maxmalipo
Ukiona kibao cha maxmalipo ...ingia wape mita namba, watakupa karatasi ya token.

Njia hizi hazina foleni.

Mwenye swali aulize! Ukikaa folen umetaka mwenyewe.
Ndio namaliza kuwapigia promo Hawa watu!! Sitaki malipo ya promo hii

Ungesoma comments za wenzako kwanza kabla ya kutoa yako, ukifuatilia kuanzia juu utagundua tatizo sio watu kufahamu hizo njia, tatizo ni mtandao na kuna mtu akaweka clear kabisa kwamba inabidi watu wakanunue kwenye vituo vya TANESCO ambavyo ni vichache! Hizo njia zinajulikana!
 
Amekurupuka tu huyu. Mimi hapa home leo ndio kulala gizani. Duh hii ni hatari.
 
Jamani naomba kuuliza kuna tatizo gani mbona mtandao wa LUKU haufanyi kazi toka jana hadi leo?

Wanaponiacha hoi ni jinsi walivyo hodari wa kupokea pesa kwenye mtandao wao halafu wanakula ganzi! Bora kama mtandao ni mbovu na pesa isiende taona mimi mwenyewe kama nisubiri au nikailipue tungi.
 
Siku nyingine muwe mnanunua units nyingi, zikikaribia labda siku 5 kuisha ongeza units zingine.
 
Kupanga ni kuchagua ...umeamua mwenyewe kukaa foleni.
Zifuatazo ni njia mbadala

1. Mpesa
Wewe kama ni Mteja wa mpesa, tigo zantel au airtel unakaa kitandani kwako unaingia kwenye menyu unanunua umeme unapewa TOKEN na kusimama, elekea kwenye mita yako tia umeme.
FOLENI UMEITAKA MKUU

2. CRDB BANK
wewe kama ni Mteja wa benki ya crdb kuna njia kuu2
i. Ingia menyu yao kwa *150*03# ingia kwenye Akaunti yako nunua umeme then unapata token ukiwa apo apo chumbani kwako.

ii. Tafuta wakala yeyote wa crdb mwambie hela hii apa nataka umeme ...ataingia kwenye machine yake na kukupatia risiti yenye token
Wakala wa hii benki nawaona kila mtaa, mtaani kwetu wapo wa3 ....
Office nyingi za posta ni wakala wa crdb.

Mwisho:
Maxmalipo
Ukiona kibao cha maxmalipo ...ingia wape mita namba, watakupa karatasi ya token.

Njia hizi hazina foleni.

Mwenye swali aulize! Ukikaa folen umetaka mwenyewe.
Ndio namaliza kuwapigia promo Hawa watu!! Sitaki malipo ya promo hii

mtoa thread anahoji kuna tatizo gani kwenye mtandao wa luku tangu jana? Njia zote ulizotaja tumejaribu zimegoma.
 
Kama hujafanikisha kupata umeme tumia njia zifuatazo nunua kwa M-pesa timia cm ya wakala itanunua ukishindwa nijurishe
 
Back
Top Bottom