Mtandao wa kijamii wa wanafunzi na waalimu

Liston Cosmas

Member
Mar 4, 2015
12
11
Habari wana JF.

Natumaini nyinyi nyote mnaendelea vyema wakati huu wa janga la COVID-19. Kwa kujitambulisha kwanza, mimi ni kijana Mtanzania na kwasasa ninasomea Shahada ya Uhandisi wa Umeme na kompyuta (Bsc. Electrical and Computer Engineering) nchini Marekani. Hivi majuzi nimemaliza kutengeneza mtandao wa kijamii ambao unalenga kuwasaidia wanafunzi wa ngazi mbalimbali, waalimu na vijana kwa ujumla.

Mitandao ya kijamii ni jukwaa la teknolojia ambao husaidia kuunganisha watu pamoja, kutoka mbali na karibu. Inatumika kujenga uhusiano kati ya watu. Matumizi ya mitandao ya kijamii na wanafunzi husaidia kupata habari haraka iwezekanavyo. Imebainika kuwa vyombo vya habari vya kijamii vina njia pana na ya haraka kusambaza habari sio tu kwa wanafunzi wa taasisi lakini pia kwa umma.

Wakati janga la COVID-19 bado linaendelea na hatujui ni lini litakwisha, niliamua kuunda mtandao wa kijamii ambao unafanya kazi kama mitandao mingine ya kijamii, lakini nimezingatia haswa mahitaji na huduma maalum za vijana; kama vile kutoa njia ya kusomea na kuwaunganisha na fursa tofauti. Mtandao huu wa kijamii nimeuita anza.

anza husaidia wanafunzi kujifunza mtandaoni kwa kutumia jukwaa la kujifunzia. Wanafunzi na waalimu wanaweza kutumia huduma hii kwa usimamizi, uhifadhi nyaraka, kufuatilia, kuripoti, na utoaji wa kozi za masomo, au programu zingine. Mwalimu ana udhibiti wa wanafunzi na kozi, kama vile, kubadilisha maendeleo, kusafisha data, nk. Mwanafunzi anaweza kujiandikisha katika kozi (au kuandikishwa na mwalimu), na kuanza kujifunza kwa njia ya mpangilio, kupitia notes, na majaribio mbalimbali katika kozi.

Kuna vikundi vingi ambavyo wanafunzi wanaweza kutengeneza na kujiunga katika jukwaa la anza. Kujiunga na vikundi hivyo kutasaidia wanafunzi kupata habari bora. Habari kama hiyo inajumuisha fursa kama masomo ya nje ya nchi na udhamini tofauti wa vyuo vikuu. Kwa kuwa mimi binafsi nilipitia mchakato wa maombi ya nje ya vyuo vikuu (na vijana wengi wanapitia hayo), ninaelewa jinsi wanavyoweza kukata tamaa, kwani ni vigumu kupata watu watakaokusaidia kweli.

Kwa hivyo kupitia mtandao wa anza, wanafunzi wataweza kushirikiana na kusaidana na watu kama mimi ambao tumeshapitia njia hii. Ushirikiano ndio njia bora ya mafanikio! Ikiwa unatafuta nafasi ya undergrad, Masters, au Ph.D., tembelea tovuti yetu. Kila kitu ni 100% BURE. Natumaini jukwaa hili litawasaidia wengi. Kama una swali lolote, ama ungependa kufanya kazi na mimi kwa namna yoyote ile, naomba unitafute kwa namba zilizo kwenye picha hiyo hapo chini. Asante, na jilindeni vyema!

5f0c036e-7b5b-4ba2-a9bb-39d370868821.jpg
 
Back
Top Bottom