Mtaji wa milioni 4

newbeliever

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
248
48
Wanajamii naomba msaada wenu katika hili.
Mimi ni kijana nakaa Dar es salaam nasoma ila nimebahatika kupata mtaji kiasi hicho tajwa hapo juu.ni mkopo toka bank. Mimi nilifikiria kufungua mgahawa hapa Dar ila sasa napata mawazo na wasiwasi kuhusu mambo ya risk e t c.
Kuna washauri humu ndani walikuwa wanasema kuwa inatakiwa mtu usiweke mayai yote katika kapu moja.sasa naomba msaada wenu kwa wenye uzoefu maana najua huu ni mtandao wa watu wenye elimu zao,wafanyabiashara,wenye uzoefu na wengine wengi.
Je niitenge vip hii hela ili niwekeze hapa Dar katika biashara tofauti tofauti ili nisije kupasua mayai yote kwa wakati mmoja? AU vip hii biashara ya mgahawa itaweza kunilipa na kufanya marejesho kwa mwezi maana natakiwa kurejesha almost laki tano kwa mwezi.Pia kama kuna mwenye ushauri wowote naomba mnisaidie katika hili maana ndo naanza biashara na ndo naanza kujitegemea.umri ni miaka 24.
Asanteni,nawasilisha
 
Mgahawa utakukipa..hapo kikubwa ni location na ubora wa huduma zako!!
 
kuanza biashara mpya kwa mkopo ni risk kubwa sana, kwa kua biashara mpya lazima uipe grace period lakini mikopo mingi huwa haina grace period, labda kama mkopo wako una grace period
 
Hamna grace period yaan ndo naanza upya.na mkopo naanza kulipa first month!!!
 
Wanajamii naomba msaada wenu katika hili.
Mimi ni kijana nakaa Dar es salaam nasoma ila nimebahatika kupata mtaji kiasi hicho tajwa hapo juu.ni mkopo toka bank. Mimi nilifikiria kufungua mgahawa hapa Dar ila sasa napata mawazo na wasiwasi kuhusu mambo ya risk e t c.
Kuna washauri humu ndani walikuwa wanasema kuwa inatakiwa mtu usiweke mayai yote katika kapu moja.sasa naomba msaada wenu kwa wenye uzoefu maana najua huu ni mtandao wa watu wenye elimu zao,wafanyabiashara,wenye uzoefu na wengine wengi.
Je niitenge vip hii hela ili niwekeze hapa Dar katika biashara tofauti tofauti ili nisije kupasua mayai yote kwa wakati mmoja? AU vip hii biashara ya mgahawa itaweza kunilipa na kufanya marejesho kwa mwezi maana natakiwa kurejesha almost laki tano kwa mwezi.Pia kama kuna mwenye ushauri wowote naomba mnisaidie katika hili maana ndo naanza biashara na ndo naanza kujitegemea.umri ni miaka 24.
Asanteni,nawasilisha

Ndugu kwanza hongera kwa ujasiri na uamuzi uliochukua wa kutaka kuwa mjasiliamali.Labda kwa kukushauri tuuu,hiyo biashara wala usiogope kuifanya yaan ianze fasta na usisite chochote, watu wengi wanaogopa kuwa wajasiliamali kwa sababu ya risk.lakini amini usiamini HAKUNA BIASHARA YOYOYTE DUNIANI ISIOKUWA NA RISK NA KUPATA HASARA NI JAMBO LA KAWAIDA!!!
Fanya iyo biashara fasta ili ikupe experience ya kupata hasara na ikukomaze ili upate ujasiri wa kuwa risk taker...ngoja nikupe historia yangu kidogo may be unaweza ukajifunza kitu;
miaka mi 4 iliyopita nilipata kamtaji kangu kidogo tu na nikawa na dream ya kuanza biashara ya kusupply matunda katika soko moja,hivyo niliwaza sana naanzaje kuingia katika biashara hii,huwezi amini pamoja na personality niliyokuwa nayo nilichukua maamuzi magumu sana ambayo hata mke wangu kipindi hicho hakujua kwanini niliamua kufanya vile,nilivizia fuso moja linaloleta matunda pale sokoni nikaomba kuwa tanboy bila ya malipo yoyote yale,dereva alinikubalia na nikaanza kupiga mzigo kama kawa,fuso naenda nalo shambani tunapakia mzigo tunaleta sokoni tunashusha tunauza,ivyo ivyo mtoto wa kiume ndo ikawa mchezo wangu wa kila siku..Kichwani nilikuwa najifunza mengi na kupata experience ya biashara ile..Kwenda na fuso shambani (ilinipa mwanya wa kufahamiana na wakulima,bei ya kununulia pamoja na connection zote za source ya matunda yangu), Kusafirisha mzigo na fuso hadi sokoni (ilinipa mwanya wa kujua gharama za usafirishaji na changamoto zake njiani)..kushusha mzigo sokoni ( nilipata mwanya wa kuwafahamu wanunuzi wa matunda,bei ya manunuzi n.k) Baada ya miezi 6 ya kuteseka na utanboy bila kulipwa ndipo nikaanza rasmi kazi iyo,aiseee nilikuwa natirirka tuuu maana nilikuwa nimeshaifahamu nje ndani na connection za wadau zote ninazo na nilikuwa tayari nimeshajenga urafiki nao.. Leo hii naandika haya nipo mbali sana na inshallah mungu akijalia mwezi wa 5 ntakuwa namalizia deni langu nililochukua benk kwa ajili ya kununua fuso langu mwenyewe. Namshukuru mungu saivi namimi namiliki shamba langu mwenyewe,fuso langu mwenyewe na nimetoa ajira pia kwa vijana wengine.
Kila la kheri katika uamuzi wako mkuu,USISITE ANZA SASA NA DREAM BIG,BAADA YA MIAKA KADHAA HUENDA UKAMILIKI HOTEL KABISA.Mungu akusaidie.
 
Umeongea poa sana
 
Hongera sana kwa kuweza kupata hiyo hela, nakushauri uwekeze kwenye bodaboda uendeshe pekee yako hela nyingne weka kwe mfuko wa UTF hutajuta , uwe unapga vichwa vya bodaboda huku unasoma, huku una akiba yako katika huo mfuko wa hifadhi
 
Hello...za jioni, wazo lako la restaurant ni zuri kama ukizingatia quality ya services zako. Kuna mtu namjua alikopa 20m na kununua machine za kupikia na alikwama, my point is its a risky business you have to invest your time, energy and money in it. Plus kwa biashara hiyo kukua inategemea na location and how you sell your products. Kuna restaurants au vibanda vingi Dar vinauza chips kuku,mayai na mishkaki na vinafanya vizuri sana..
 
Kaka nashukuru sana sana sana,yaan umenipa moyo sana.Kiukweli nina nia ya dhati sana pia nimepania sana katika kuboresha huduma! Ila nilikuwa nasumbuliwa na wasiwasi huo.nitainvest mda wa kutosha sana na nitakuwa very serious na kazi.Kaka nawe hongera sana maana umepiga hatua sana! mungu azidi kukuongoza na kukujalia
 
Hongera sana kwa kuweza kupata hiyo hela, nakushauri uwekeze kwenye bodaboda uendeshe pekee yako hela nyingne weka kwe mfuko wa UTF hutajuta , uwe unapga vichwa vya bodaboda huku unasoma, huku una akiba yako katika huo mfuko wa hifadhi
Samahan kaka, mie sijui kuendesha boda boda ila nashukuru sana kwa ushauri wako.pia kaka kuhusu huo mfuko wa UTF unafanyaje kazi na mapato yake yako vip?
 
Hello...za jioni, wazo lako la restaurant ni zuri kama ukizingatia quality ya services zako. Kuna mtu namjua alikopa 20m na kununua machine za kupikia na alikwama, my point is its a risky business you have to invest your time, energy and money in it. Plus kwa biashara hiyo kukua inategemea na location and how you sell your products. Kuna restaurants au vibanda vingi Dar vinauza chips kuku,mayai na mishkaki na vinafanya vizuri sana..
Ni kweli ndugu cha muhimu ni kupata location nzuri na frame nzuri,quality service, time investment etc.ila nimejipanga katika hilo maana najua hela nimeipata kimkopo mkopo
 
Samahan kaka, mie sijui kuendesha boda boda ila nashukuru sana kwa ushauri wako.pia kaka kuhusu huo mfuko wa UTF unafanyaje kazi na mapato yake yako vip?
Bodaboda unajifunza siku moja tu mkuu unakuwa tayari upo vizuri,unaanza kula vichwa huku unaendelea na mambo yako mengne
 
Tenga TZS 128,500 wekeza kwenye mradi wa Rifaro. Zinginezo wekeza kwenye mradi utakaoamua kuufanya. Ni vyema kuwa na biashara tofauti wakati mmoja ili kupunguza risk ya kuwekeza kwenye mradi mmoja kwani ukishindikana basi na mtaji wako wote umekwenda.

Biashara ya kuwekeza kwenye mradi wa Rifaro haina gharama zingine zaidi ya kulipia mtaji wa TZS 128,500 tu na ni biashara ambayo hata kama uwe mzito kiasi gani huwezi kupata hasara kwani lazima hela yako itarudi kadri siku zinavyokwenda.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu wa Rifaro, soma thread hii

Kwa nini utumie simu yako ya mkononi bila kulipwa wakati kuna Rifaro?
 
Mkuu kimsingi mimi ni mwanafunzi kama ww, na nimeshawahi kujaribu kugusa baadhi ya biashara ikiwemo kibanda cha chipx ambapo uendeshaji wake unauhuiano mkubwa na mgahawa, mind you rafik yangu, pesa ya mkopo sio ya kuanzishia biashara risk km ya mgahawa ukizingatia bado unasoma, biashara ya mgahawa inakuhitaji kuliko ww unavyoihitaji, huwezi ukafanikiwa katika biashara hiyo kwa kuachia watu waiendeshe,
Naweza nikasema asilimia 90 ya biashara yoyote ambayo unaanzisha halaf hauna muda wa kua karibu nayo utapoteza pesa yako ukizingatia ni pesa ya mkopo, binafsi kwa uzoefu wangu dnt the risk, biashara ya chakula kuna siku unaweza ukaamka wafanyakaz wamegoma kuja kazini ww upo chuo unafanyaje?
Jitafakar tena kisha fanya utafiti wa kina ndg yang,
Sasa ni biashara gan ambayo naweza nikakushaur ufanye? 1. Uuzaji wa magodoro, biashara hii hata ukiwa unasoma moshi yenyewe ipo dar mtu hawezi kukuibia ingawaje unatakiwa uweke mtu ambae hana uwezekano wa kukimbia na mtaji.
2. Biashara ya vinywaji, vya jumla, biashara hii hata ukimuweka mtu ukaendelea kusoma bidhaa zake zinahesabika na ni ngumu kukuibia, ingawaje hii itakuhitaji katika kuweka mbinu za masoko, za mauzo na promosheni mbalimbali,
3. Furniture, hii ni biashara ambayo unaweza ukaanza nayo kwa mtaji mdogo lkn ukakua kdg kdg na biashara hii hata ukiendelea kusoma ukaweka mtu furniture zitauzika 2 na mahesabu utakua nayo mkononi.
4. Usafiri, hapa namaanisha bajaji, tafuta kilema mnunulie bajaji muwekee pale posta feli utapiga pesa bila stress nyng kichwan ingawaje ukiweka mtu muhuni hii biashara utaijutia sana, tafuta mtu makini, na mwaminifu mkuu..

Mwisho katika kila biashara utafiti, utafiti, utafiti ni muhimu sana, usikae kuchat na kushinda instagram nenda kazungumze na watu huko nje, fanya utafiti wa biashara inayokuvutia kwa watu ambao tyr wanazo n. K itakusaidia sana
 
Back
Top Bottom