Mtaji Kilimo cha Umwagiliaji

JT wa Dommy

Member
Sep 15, 2016
29
38
Habari wa JF. Mimi ni binti ambaye nataka niingie shambani kuanza kilimo. Msaada wenu nauhitaji kujua gharama nzima ya kulima kilimo cha umwagiliaji. Kuanzia ukodishaji shamba hadi vifaa vya umwagiliaji pia maeneo gani mazuri na zao gani zuri lenye kuleta faida na gharama za mbegu. Kwenye maeneo sichagui maana nimeamua kuingia shambani hata mikoani nitaenda tu. Asanteni
 
Una umri gani kwanza maana kilimo ni mojawapo ya magonjwa ya presh kama utakuwa umekopa hela bank alafu ukalima nyanya then ukaotea msimu kreti la nyanya 700/=
 
Habari wa JF. Mimi ni binti ambaye nataka niingie shambani kuanza kilimo. Msaada wenu nauhitaji kujua gharama nzima ya kulima kilimo cha umwagiliaji. Kuanzia ukodishaji shamba hadi vifaa vya umwagiliaji pia maeneo gani mazuri na zao gani zuri lenye kuleta faida na gharama za mbegu. Kwenye maeneo sichagui maana nimeamua kuingia shambani hata mikoani nitaenda tu. Asanteni
Gharama za kilimo zinatofautiana kutokana na aina ya mazao na sehemu inayoenda kulima,kwa mfano ukilima nyanya sehemu za Morogoro zinaweza kukugharimu 1,500,000.Tsh.kwa mbegu aina ya Assila F1.
 
Kwa uzoefu wangu nyanya zina soko zuri mwezi wa kumi na mbili mpaka mwezi wa saba ambapo huwa zinaporomoka bei vibaya mpaka wanaishia kulishwa ng'ombe kama tunavyoonyeshwa kwenye mitandao.
Hivyo basi miezi mizuri ya kuandaa kitalu ni mwezi wa saba mpaka wa pili mwishoni. japo miezi ya kwanza na pili nyanya zinapolimwa mazingira yenye joto sana usitegemee kuvuna kutokana na maua kupukutishwa na joto labda kama unatumia technogy ipasavyo kama greenhouse au vitu kama multching vinaweza kukuokoa.
 
Habari wa JF. Mimi ni binti ambaye nataka niingie shambani kuanza kilimo. Msaada wenu nauhitaji kujua gharama nzima ya kulima kilimo cha umwagiliaji. Kuanzia ukodishaji shamba hadi vifaa vya umwagiliaji pia maeneo gani mazuri na zao gani zuri lenye kuleta faida na gharama za mbegu. Kwenye maeneo sichagui maana nimeamua kuingia shambani hata mikoani nitaenda tu. Asanteni
hongera kwa kuchagua kilimo and i hope umefanya uchunguzi mzuri nasio kuvutiwa na story za lakimbili kuwa milioni tano,
kamakweli unataka mafanikio kwenye hii industry [na ndio ushaamua kuingia shamba] kwanza kabisa chagua zao unalolitaka then fanyia uchunguzi mzunguko wake yan kipindigani linakua na thamani zaidi fanya hesabu afu ingia mzigoni kifupi usikurupuke itakusaidia kuepuka majuto,
kwakumalizia jitahidi kufanya kitaalam zaidi, shirikisha zaidi wataalam usipende kuskiza story zawatu hasa kuhusu madawa na mbegu
all the best of luck.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom