Mtaji kiasi gani utatosha kuanzisha kampuni ya ulinzi?

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,382
1,208
Nina mpango wa kuanzisha kampuni ya ulinzi taratibu zote nazijua isipokuwa nataka nijue natakiwa kuwa na pesa ngapi kama mtaji ili lengo langu litimie? Karibuni wadau wakati ndo huu.
 
Nazan ungeshare kwa kile unachokijua kwanz ili na wengine wapate ujuz then na wengeni watakuja kushusha nondo
 
Nina mpango wa kuanzisha kampuni ya ulinzi taratibu zote nazijua isipokuwa nataka nijue natakiwa kuwa na pesa ngapi kama mtaji ili lengo langu litimie? Karibuni wadau wakati ndo huu.
Wateja wa aina gani unawalenga ?

Maana,

Kuna kampuni za ulinzi zina malindo mpaka ya bar, grocery, vituo vya mafuta uswahilini, maduka ya watu n.k

Na kuna,

Makampuni yana malindo kwenye Mahotel makubwa ya kitalii, makampuni makubwa, migodini, magodown, mabandari, Airports, mabenk n.k

What's your targetted Niche ?

Where have you spotted a gap ?
 
Inategemea unataka kampuni yako inataka ijishughulishe na wateja wa aina gani, hapo ndio utaweza kuweka makadirio ya huduma unazotakiwa uwe na uwezo wa kuzitoa. Mfano wengine wanataka walinzi wawe na silaha za moto, mbwa, mitambo ya CCTV na Intruder, pia wako makini kuchagua vigezo na uzoefu wa askari wako, hii inamaanisha utaajiri waliosoma kiwango cha kuridhisha.
Ukiwa na wateja wa aina hiyo, lazima uwe na pesa ndefu kidogo, hapo hatujaongelea magari ya kurahisisha ufanyaji wa kazi achilia mbali wafanyakazi watakao kua ofisini kuratibu mambo yote. Weka na gharama za kukodi ofisi na mambo mengine ya muhimu kwa kuanzisha ofisi.

Lakini unaweza kuwa umelenga wateja wa kati na wa chini ambao wanachohitaji wao ni mtu wa kuwaangalizia nyumba tu, hawahitaji cha radio call, emergency and rescue, magari, na mambo mengine, hapo kunakua na unafuu.

Kumbuka siku zote penye nia pana njia mkuu. Kila la kheri
 
Wateja wa aina gani unawalenga ?

Maana,

Kuna kampuni za ulinzi zina malindo mpaka ya bar, grocery, vituo vya mafuta uswahilini, maduka ya watu n.k

Na kuna,

Makampuni yana malindo kwenye Mahotel makubwa ya kitalii, makampuni makubwa, migodini, magodown, mabandari, Airports, mabenk n.k

What's your targetted Niche ?

Where have you spotted a gap ?

We jamaaa weweeeee! Umenifurahisha sana mkuu, inaonekana tulikua tunaandika wakati mmoja. Nimependa sana ulivyoweka vizuri post yako. Imeelezea kitaalam kitu nilichokua nakiwaza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom