Mtahiniwa Kidato 4 ajinyonga

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
57
MWANAFUNZI wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Mwapachu iliyoko Kata ya Tangasisi jijini Tanga amekufa baada ya kujinyonga usiku kwa kutumia kamba ya manila.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa yatima, amefahamika kwa jina la Sudi Omari (19) mkazi wa Mwakidila ‘A' na kabla ya kujinyonga juzi alikuwa tayari amefanya mitihani mitano ya kumaliza kidato cha nne iliyojumuisha masomo ya Hisabati, Uraia, Jografia, Kiswahili na Baiolojia. Mitihani ya kidato cha nne inatarajiwa kumalizika Oktoba 22 mwaka huu.

Ofisa Upelelezi Mkoa wa Tanga, Jaffari Mohammed akithibitisha tukio hilo ofisini kwake jana na kusema tukio hilo lilitokea Oktoba 6, mwaka huu baada ya mama yake mlezi wa Sudi kuingia chumbani saa 12.30 asubuhi na kukuta akiwa amejitundika darini.

"Ni kweli tumepokea taarifa ya kujinyonga kwa mwanafunzi aliyekuwa akisoma kidato cha nne katika Sekondari ya Mwapachu na alitumia kamba ya maila chumbani anakolala ila mpaka sasa bado hatujapata chanzo uchunguzi unaendelea," alisema.

Kwa upande wake Ofisa Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, Kassim Sengasu akizungumza katika mahojiano na HABARILEO alisema tukio hilo limemsikitisha sana hasa kwa kupoteza kijana ambaye darasani alikuwa na uwezo mkubwa.

"Juzi (jana) mchana nilipokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Mwapachu aitwaye Cornel Rambau akinijulisha kuwa Sudi hakufika kwenye mtihani wa somo la Historia uliofanyika siku ya Jumatano mchana kwakuwa amefariki baada ya kujinyonga na hivyo yeye anakwenda kutazama maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo na nikaamua kuambatana naye," alieleza.

Sengasu alibainisha kuwa Sudi ambaye ni yatima tangu alipokuwa darasa la kwanza alikuwa akiishi na mama yake mdogo, Manahuru Athuman huko Mwakidila, lakini alikuwa akipata msaada kutoka kwenye taasisi isiyo ya kiserikali ya kusaidia yatima iitwayo AFRIWAG yenye makazi yake jijini hapa.

Ofisa Elimu huyo aliongeza kuwa pamoja na kuwa yatima Sudi ni miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakifanya vizuri darasani na kwamba shuleni hapo alikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache wanaotarajiwa kufaulu mtihani huo kwa kupata daraja la kwanza au la pili.

Naye Mwanahuru aliyekuwa mlezi wa kijana huyo, alisema hadi majira ya usiku walishiriki chakula cha usiku pamoja na kila mmoja aliendelea na shughuli zake, majira ya saa kumi usiku walisikia kelele za baiskeli kama ikigongwa wakahisi kuwa labda ni mwizi.

Mwanahuru alisema baada ya hali hiyo kuendelea kwa muda jirani yao alianza kumwita marehemu, lakini kimya kilitawala hali iliyowaingiza hofu ambapo waliamua kwenda chumbani kwa marehemu na kumkuta akining'nia huku anatoa sauti ya kukoroma.

Sudi alizikwa jana mchana baada ya sala ya Ijumaa kwenye makaburi yaliyoko eneo la Mapinduzi katika Kata ya Tangasisi katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.
 

Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,592
5,336
Ooooh, hivi itakua ni despair gani imempeleka kufanya hivo wakati he seem to have such a promissing future? Masikini... RIP.
 

Natalie

Senior Member
Sep 25, 2011
165
27
Mh, inasikitisha sana, au alihisi kuwa hakufanya mitihani hiyo vizuri kama alivyotaka au alikuwa amepanic kwenye mitihani akahisi hatofauli vizuri kama inavyotakiwa na si ajabu akose mybe sponsorship aliyoitegemea baadaye, kuna wengine wanaolipiwa na maNGO's unakuta wanahaidiwa kwenda kusoma Ulaya wakipata division fulani, maybe one or two ya mwanzo, sasa wakiona dalili ya kutoweza kufaulu hivyo maybe kwasababu mitihani imekuwa migumu zaidi au walikuwa wamepanic kwenye mitihani, wanachanganyikiwa sana, but inawezakana ikujulikana kilichomfanya ajiue, kama sisi binadamu hatutajua, yeye na Mungu ndio wanaojua hiyo sababu. R.I.P huyo kijana.
 

Natalie

Senior Member
Sep 25, 2011
165
27
La kwanza mpaka form four kama yatima, leo hii ndio anakata tamaa, hata kama ingekuwa uyatima wa form one mpaka form four, unakula ng'ombe mzima unaacha mkia, kufeli, unaweza kuresit, na kufeli shule si kufeli maisha, tusikate wala kukatishwa tamaa na mtu, hangaika kadri ya uwezo wako, kufanya maisha yako kuwa mazuri, we ndiye mpiganaji pekee wa kuboresha maisha yako yawe mazuri, tusikate tamaa, Mungu atatuongoza na kutusaidia, pepo la kukata tamaa lishindwe.
 

Kanyigo

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
1,028
188
sasa huyu kijana walimdanganya kwamba majibu aliyoweka sio sahihi au alijuaje? R.I.P KIJANA.
 

Rashdind

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
201
60
Madogo wa kidato cha 4 ata kama mkihisi amkufanya poa kamwe msichukue uamuz mbovu ka huo pepa ikizingua sio mwisho wa maisha njia za kutokea ziko nyingi tu na sio wote wanaofaulu ndo wanatoka kimaisha, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 

zamlock

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
3,841
650
jaman ametangulia mbele za haki, sina cha kusema kwa sababu angekuwa hai na maamzi hayo aliyochukua ningemshauri asifanye hivyo kwa sababu ni dhambi lakini kwa sababu amesha chukua maamzi na atuko naye tena basi sina jinsi juu ya kumweleza kuwa ni maamzi mabaya sana aliyochukua ingawa awezi upata huu ujumbe basi itakuwa ni faida kwa wengine ambao wanaweza chujua maamzi kama haya kuwa kujinyonga ni dhambi mbele za mwenyezi Mungngu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom