Mtafute MUNGU wako kuliko pesa.

Mtafute MUNGU wako kuliko pesa.

Ryan The King

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
2,789
Reaction score
2,706
Amani itawale!.

Andiko hili ni kwa wenye kuutafuta uzima wao, wenye kutaka kujua ilipo hatima ya roho zao. Basi isomeke kwa hekima kwa wale wenye hiyo hekima na upumbavu kwa walio wapumbavu.

Masikini binadamu umegeuka na kushindwa kuelewa mambo madogo. Unahangaika kwa mambo yasiyo na faida. Nawe hujui kilicho mbele yako.
Ukasahau uendako ni ugenini na muda wako hapa duniani ni mchache.

Umejidanganya na vitu vya mchanga ambavyo navyo siku moja vitarudi kuwa udongo. Unahangaika Kama hayawani wasio na akili, tena bora hao hayawani wanaomkumbuka Mungu wao na kufanya ibada kila siku lakini wewe umejitia kibri katika nafsi yako. Nawe wasema nafsini mwako hakuna Uzima usijue upo ugeni huko uendako.

Muda wako ni mfupi Sana na mapito yako ni Kama moshi. Hupita kwa kasi. Nawe hujui yakuwa utarudi mavumbini kwa ghafla. Basi angalia na ujiandae kwa maana huko uendako ni ugenini.

Wengi hushindwa kujiandaa katika siku ile. Siku yenye Giza kuu, siku ambayo mwili wako wenyewe utakusaliti. Macho yako yatakosa nuru, ubongo wako utakosa fahamu, nayo sauti yako itafungwa ping isitoke. Utatamani uongee lakini muda utakuwa umeisha.
Hakika uendako ni ugenini kujiandaa ni muhimu ewe Mwanadamu.

Safari hii ni yako mwenyewe. Hakuna utakaye msingizia kwa lolote katika siku ile. Kila mmoja ataongea mambo yake mwenyewe aliyoyasema, yafikiri na kuyatenda.

Basi ewe mwanadamu usijitie ujuaji kwa mambo usiyokuwa na hata chembe ya ujuzi usije ukajitia katika hukumu mwenyewe.

Mtafute Mungu wako kuliko pesa, kwani huyo ndiye mtetezi wako hapa duniani na huko ugenini usiko kujua.
Pesa haitakusaidia lolote ewe Mwanadamu, pesa haijawahi kumsaidia yoyote katika siku ile. Wengi walihadaiwa na Mali za dunia wakajikuta katika bahati mbaya iliyowajia kama ajali. Walikufa bila Kujiandaa nao wasijue huko waendako pesa haina kazi yoyote. Basi wapo katika majuto makuu na watasema laiti tungelijua tungekutafuta ewe MUNGU mtakatifu kuliko pesa.

Huko ugenini tuendako hakuna cha kununua ndugu wanadamu. Hangaika kumtafuta Mungu kabla siku ile itakapofika siku ya ghafla.

Kaburi halitajali wewe ulikuwa ni tajiri wala masikini. Msomi au mjinga, Kiongozi au mtumishi nakadhalika.
Litakutambua Kama abiria katika siti yako ya mchanga. Hata ujaribu kuweka marumaru na saruji au hata chokaa katika kaburi lako lakini kaburi halitakuwa na huruma na wewe. Lazima uelewe yakuwa uendako ni ugenini.

Kama ulivyokuja duniani hukujua kuwa ni nani utakaye kutana Naye, nani atakuzaa basi huko uendako ndivyo kulivyo. Yapaswa maandalizi makubwa Sana.

Mtafute MUNGU kuliko pesa.

~Michaelray
 
Bora watu watafute pesa kwanza sababu ndizo zinazopatikana maana zipo.

Mtu ukishakuwa na pesa 99% ya shida zako zinaisha, hata huko makanisani mkihudhuria kwa mwezi mzima bila kutoa pesa lazima wafunge makanisa.

Imeandikwa tafuteni ufalme wa Mungu kwanza na mengine mtapewa kama ziada lakini mimi nawambieni tafuteni pesa kwanza maana pesa ndio kila kitu.
 
Duh, kweli wanadamu tunaangamia kwa kukosa maarifa, mleta mada wachache sana watakaokuelewa juu ya kiwango chako cha maarifa maana wengi wao ni fuata upepo!
Mkuu, upo ktk himaya ya Mungu wakati wote ikiwa unasadiki kila ukionacho na usichokiona kwa macho yako kimefanywa na yeye! Unadhani mwanadamu umepotea? Umepotea ukawa kwenye mamlaka na himaya ya nani? Hakuna mamlaka izidiyo mamlaka na Mungu na hakuna aliyefanya himaya ktk himaya ya Mungu!
Kama jinsi ambavyo mwanadamu hukuamua uzaliwe wapi na nani, hayo yote aliyafanya na kuyaamua yeye, hivyo ndivyo Mungu ajuaye hatima yako huko udhaniako ugenini! Mwanadamu huna ujanja hata tone ya kujiondoa ktk mamlaka na himaya ya Mungu! Yote unayoyaona na yanayotokea ni mipango ya Mungu mwenyewe ktk kujitukuza juu ya ukuu na uweza wake! Wewe enenda unavyoweza ili ktk kipindi hiki kifupi duniani usiwe msindikizaji, chaguo la mwenendo wako ulijue maana linaweza kukuwahisha kukufikisha ktk ukomo wa uwepo wako hapa Duniani ama kukufanya ukawie na kuishi miaka mingi!
Wanadamu tumepewa mamlaka juu yetu wenyewe Ndio maana tunazo mahakama kwa ajili ya sisi wenyewe kujisimamia ktk chaguzi zetu za maisha ziwe za haki bila kuwaonea wengine, usimamizi huu upo juu yetu wanadamu!
Cha msingi sana hapa Duniani ni hiki, tufundishane kuijua haki, kweli na wajibu, tupende haki, kweli na wajibu, na tutende ktk haki, haki na wajibu!
Masuala ya kumtafuta Mungu yapo ktk kuijua haki, kweli na wajibu na kupenda kutenda ktk haki, kweli na wajibu na ieleweke kuwa, Mungu hapotei kiasi cha mwanadamu kumtafuta! Kama jinsi uonavyo maisha yanaendelea duniani, basi ndivyo uwepo wa Mungu unavyojidhihirisha! Haijalishi viumbe vinatenda nini, yote hutendwa kulingana na wakati wake! Viumbe hatuna uwezo wa kupingana na wakati, wakati umefanywa na Mungu mwenyewe hivyo ajuae zaidi ugenini kwako baada ya maisha ya hapa duniani ni Mungu mwenyewe kulingana na namna alivyoamua uishi mazingira gani wakati wa uhai wako duniani!
Nimependa uzi wako kwa kuwa hujaegemea dini yoyote ktk maelezo yako nami nimeeleza pasipo kuegemea dini yoyote bali ni ktk kutoana tongotongo za mapokeo!
 
Back
Top Bottom