Mtabiri longolongo

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165


Katika mojawapo ya sijui niite utafiti au utabiri, mwanasayansi huyo wa Ki-Irish, [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Dionysius_Lardner"]Dk. Dionysius Lardner [/ame]aliyeishi kati ta Mwaka (1793-1859) aliwahi kusema kwamba, Garimoshi halitaweza kwenda kasi hata siku moja.
Alisema garimoshi litaendelea kuwa na kasi ndogo sana, kwani likienda kwa kasi kubwa, abiria wataweza kufa kwa tatizo linalifahamika kitaalamu kama Asphyxia, yaani kukosa pumzi.

Pamoja na kwamba alikuwa ni mwanasayansi, Lakini nadhani alikuwa hajui anachokisema kwa wakati ule.

Kwa nini?

Kwa sababu leo hii kuna magari moshi yanayosafiri hata kilomita 500 kwa saa.

Sasa sijui mwanasayansi huyu alikuwa anatumia ubongo huu tulio nao katika tafiti zake au alikuwa anatumia nini, mimi sijui.


 
Back
Top Bottom