Mtaalamu wa umeme saidia hapa

Humary

Member
Jan 31, 2014
61
77
Habari zenu wanajamvi..! Huko mkoani kwetu (Ruvuma) kuna mradi wa umeme unaoendelea kujengwa kutoka Makambako kwenye gridi ya taifa kuelekea mkoa wa Ruvuma. Njia hiyo ya umeme itakuwa na msongo wa kv 220.

Ninachohitaji kujua ni kama hizo kv 220 zinatosheleza mahitaji ya viwanda kama sera ya taifa inavyotaka au laa. Pia naomba kuuliza kiwanda kikubwa mathalani kama cha simenti kinaweza kutumia umeme kiasi gani kwa siku.

Ahsanteni.
 
Sio mjuzi ila nadhani utatosha kibabe usipotosha tutaufungulia kesi hakuna mjadala
 
Swali lako la kitoto au la kijuaji

mahitaji ya viwanda si mpaka vijulikane ni viwanda gani hasa na vina mahitaji gani?

aliekwambia Ruvuma kuna viwanda vya kutosha ku demand umeme mkuubwa nani?

Hakuna kiwanda kitakocho jengwa Ruvuma kikashindwa ku operate kisa umeme...
 
Mimi naona hata majenereta ya pale lizaboni nadhani yanaweza kuhudumia kiwanda
 
Duh Mkuu eeh kuwa upinzani sio kuuliza vitu ambavyo tayar majibu yake yatawepo.
 
Mkuu huo ni umeme mkubwa sana, tambua kuwa K.V Moja ni sawa na Volt 1,000, sasa K.V 220 ni sawa na Volt 220,000 =, sasa Mind you Volt peke yake haziwezi kuwa considered kwenye insue ya Kiwandani, kuna vitu kama hiyo Mitambo inauma Power kiasi gani katika umeme, ambapo power hupimwa kwa kutumia Watts, sasa hapo kuna hesabu nyingine za Watts katika Volt, ambapo ndo upate Power gani inatumika hapo...Subiri ma engineers Waje....
 
Naomba nikujibu kama ifuatavyo:-
220kV sio nguvu ya umeme inayotakiwa na viwanda, bali ni jinsi moja wapo ya kusafirisha umeme kwa umbali mrefu zaidi,ili kupunguza umeme usipotee mwingi njiani (voltage loss).

Na sababu ingine, 220kV inakuwezesha kusafirisha umeme kwa kutumia cable size ndogo (less current), hivyo huhitaji structure kubwa kubeba waya.

Kutosha au kutotosha kwa umeme ni ile nguvu ya kituo kitakachojengwa (Sub-station) ili kupoza huo umeme wa 220kV (ambao naamini ni wa grid) uje mpaka 33kV au 11kV kwa ajili ya viwanda.

Naamini kuna uchambuzi utakua ushafanyika ili kujua ni kiasi gani kitahitajika ila kukidhi haja ya hivyo viwanda, hivyo transformer stahiki zitawekwa, Mathalan umeme unaotakiwa ni 15MW, hivyo wao wanaweza kujenga kitua cha 20MW.

Swali lako lingekua sahihi kama ungeuliza kituo kinachojengwa cha XXMW, 220/33kV , kitatosheleza umeme wa viwanda ? hapo ingekua rahisi kukujibu.

Swali la pili, kuhusu kiwanda cha cement, swali hili halijakamilika kwani size ya viwanda vya cement ipo kuanzia range ya 5MW - 50MW, inategemeana na production capacity (tonnes/hr).

Ni hayo tuu kwa uchahche
 
Umemjibu vyema sana
 
Back
Top Bottom