PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Akizungumza kuhusu hali ya baada ya uchaguzi, Mtaalamu wa Saikolojia, Leonard Mgina amesema kuwa kuendelea kuwakamata watu kutokana na matukio yaliyotokana na uchaguzi kunachochea majeraha ya kisaikolojia na kudhoofisha jitihada za kujenga taifa lenye umoja na amani.
“Ni muhimu sasa kuelekeza nguvu katika uponyaji wa taifa. Hakuna anayepaswa kukamatwa au kutishiwa kwa sababu ya matokeo ya uchaguzi. Huu ni wakati wa maridhiano, siyo visasi,” amesmea Mgina.
Amefafanua kuwa viongozi katika ngazi zote kuanzia mkoa, wilaya, tarafa hadi kata wanapaswa kuandaa mipango ya kuwarejesha wananchi katika hali ya kawaida, kuwafariji walioumia, na kuanzisha programu za mazungumzo ya pamoja ili kujenga imani upya miongoni mwa Watanzania.
“Watu wasinyamazishwe. Katika kuzungumza ndipo uponyaji unapatikana. Mijadala ya wazi kuhusu yaliyotokea inasaidia watu kupona kisaikolojia na kurejesha umoja,” amesisitiza.