Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,455
- 32,981
MTAA WA HAMZA MWAPACHU KWALE COUNTY, KENYA
Haya kanihadithia Juma Mwapachu uso kwa macho.
Juma Mwapachu anasema alipokuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki alikutana na Ali Mwakwere.
Ali Mwakwere ameshika nafasi nyingi katika serikali ya Kenya hadi kuwa Balozi wa Kenya Tanzania.
Ali Mwakwere bila shaka kwa kusikia hii ''Mwa,'' ''Mwa,'' akamuuliza Juma Mwapachu endapo yeye ni Mdigo.
Hapo Juma Mwapachu akampa historia nzima ya marehemu baba yake Hamza Kibwana Mwapachu na kumfahamisha kuwa alikuwa Mdigo wa kwanza kuingia Makerere kama mwanafunzi.
Ali Mwakwere akamuahidi Juma Mwapachu kuwa Hamza Mwapachu anastahili kukumbukwa na atahakikisha kuwa anapewa mtaa Kwale Mjini.
Ali Mwakwere alitimiza ahadi yake na nilipokutana na Ali Mwakwere kwenye maziko ya Juma Mwapachu Tanga alinieleza kuwa watu wa Kwale wamemuadhimisha Hamza Kibwana Mwapachu kwa kumpa mtaa.
View: https://www.youtube.com/shorts/2Qb6SIHyLwY?feature=share