Msuya atueleze aliko Sokoine

Ki Mun

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
3,442
Reaction score
4,392
Tunapokaribia kuadhimisha miaka 31 tangu kilipotokea kifo kilichojaa utata cha aliyekuwa Waziri Mkuu Ndg.Edward Moringe Sokoine,ni wakati mwafaka sasa kumhoji Mh.Cleopa Msuya juu ya tuhuma za kuhusishwa na kifo cha Mh. Sokoine;kwa sababu Mh. Msuya kwa siku za karibuni amejitokeza kukemea maovu mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa CCM bila shaka pia atakuwa na ujasiri wa kujitokeza na kutolea ufafanuzi wa tuhuma hizi.
 
Mkuu Hana lolote eti anakemea ufisadi
 
Kweli zama za Mr Dhaifu , mwizi mlinda majangili na drugs lord zimekwisha. Tutasikia mengi sana.
 
Mwaka huu tutasikia mengi sana lakini kweli msuya hawezi mziki wa Lowasa hata afanyeje kama haamini amuulize Kinanan na Nape
 

nenda jukwaa la historia utapata mwangaza dogo
 
yupo kwa mungu anamaisha . yake
 
Nakumbuka kwenye kipindi cha majira (RTD) tarehe 10/4/1984 - siku mbili kabla ya Sokoine "kuuliwa", Ben Kiko aliripoti kuwa Mh. Sokoine alitamka hivi (kwenye kikao cha CCM) :-

"...Na wale Ma-Padri tuliowakamata kwenye uhujumu uchumi tutawapeleka kwa Baba Askofu wao... pia kikao kijacho tutawawajibisha viongozi wa juu wa chama na serikali ambao watabainika kuhusika na uhujumu uchumi..."

Siku mbili baadaye... Sokoine was GONE...GONE Forever....!

Kwa wale ambao mlikuwa hamjazaliwa:-

 
Mtengeti, usimkaripie. Historia hairekebishwi lakini hufundisha. Lakini pia usiwe na uhakika sana kwamba serikali mpya ijayo haitafuatilia yaliyopita hasa yenye maslahi ya taifa kama mikataba fake, ufisadi na wizi wa raslimali za taifa. Hawa tunawafahamu na tutadeal nao. Wote waliokwapua mali zetu kwa njia yoyote, zikaachwa nchini ama kupelekwa nje, tutazifuatilia. Wengine watakuwa marehemu, tutashughulika na warithi wao lengo raslimali za taifa zirudi, zifanye maendeleo ya nchi, lakini pia liwe somo kwa wanaodondosha mate wakitamani fursa za kufanya uhuni kama ule.

Kwa habari ya kifo cha Sokoine, Bwana Msuya na Kawawa ambaye ni marehemu kwa sasa, wlaikuwa kwenye system. Sidhani kama mtu akiwauliza uelewa wao juu ya jambo hilo la kifo cha Sokoine, kunakuwa na jinai yoyote.
Yeye ajibu tu anachokielewa, historia iandikwe vizuri au iwe updated. Pale atakwama, atasaidiwa.

Kwani yule mganga aliyekuwa anawaosha madawa usiku kwenye mavyungu pale kwa Msuya, ambayo yanasemekana yalimaanisha kuondoa maruwe ruwe aliyokuwa yakiwatokea baada ya kifo hicho alikufa? Kama hayupo bila shaka watoto wake bado wapo, wanaweza kusaidia pia katika uandishi wa historia hii katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi.

Hallucinations zinaweza kuwa zilikuwa zikiwapata kwa labda walimpenda sana Marehemu na kuguswa sana na kifo chake kuliko wenzao. Na ukaribu huo ndio unaotamanisha watu wasikie lolote juu ya kifo hicho kutoka kwao.


 
Karibia na uchaguzi mkuu mwaka 2010, Jenerali Ulimwengu alipata kuandika kuwa tunapoelekea uchaguzi mkuu tutarajie mengi. Watu wenye heshima zao ndani ya jamii na elimu isiyo na shaka watasimama na kuongea mambo ya hovyo kabisa kuliko neno lenyewe "hovyo" linavyomaanisha. Si kwamba hatakuwa hawaelewi kuwa wanaongea upuuzi, bali watafanya hivyo ili kutimiza haja za matumbo yao.

Alilolisema Jenerali Ulimwengu takribani miaka mitano iliyopita linajirudia leo! Watu wazima wanaongea upuuzi tu bila kujali chochote! Huyu anaongea hili yule anaongea lile yaani ujinga ujinga!

Wewe uliyeleta huu uzi bila shaka unatumia kiuno kufikiri na kama si hivyo basi tumbo lako ndilo linalokuongoza kuleta huu uozo! Sokoine kafariki lini? wakati wote huo ulikuwa wapi kuiibua hii hoja yako? Mnapenda kuleta viroja kujibu hoja nzito. so hutaki Msuya akemee ufisadi? Unataka kumchafua Msuya kisa anakemea ufisadi wa bwana wako? Mlimchafua Salim Ahmed Salim na sasa mnamchafua Msuya!

Mnapokosa hoja tulieni na sio kuleta vioja.
 
Uanjua watu wanasemaga vitu bila kujua kuna siku vitakuja kuleta maswali.

Kama kuna mtu anasema Sokoine alikuwa akiwa njiani kuelekea Morogoro, nani alithibitisha kifo cha Sokoine? Kulikuwa na Daktari kwenye ile gari aliyempima na kujua alifia njiani wakienda Morogoro?

Nini ilikuwa sababu ya kumpitisha Morogoro Regional Hospital Ikiwa walikuwa wanajua alifilia njiani hata kabla hajafika Morogoro?

Ni vizuri wakanyoosha maelezo.

Ninachokifahamu mimi, waliompeleka Hospital ya Morogoro walikataa asipimwe kwamba alishakufa. Ni jambo dogo lakini ni vizuri kuliangalia kwa upana. Pale Morogoro hakuna Daktari alimpima Sokoine kuthibitisha amekufa ama la. Dr. Materu, aliyekuwa zamu pale, aliye wapokea hakuruhusiwa ampime.

Kama ni report iliandikwa ilikuwa ni kwa formalities na kutokana na maelezo waliyokuwa wanayapata.

Ninaogopa kusema zaidi kwa hofu ya kuambiwa naandika uchochezi.

Imetosha.


 
Msuya kayataka haya....yeye na Kawawa ndio prime Suspects though ni wazi Kawawa hakuhusika...Msuya ndie aliyeliliwa na wengi na hata hayo mauzauza kipindi kile yalimhusu yeye...Mzee Rashid aliingizwa na wahuni ili Cleopa apone.

Mwalimu ali handle hii issue vyema otherwise Msuya asingelipona toka usoni machoni pa watu
 
Kifo cha sokoine kimebaki na utata mpaka kesho. Sasa watu wanataka kutumia utata huo kujinufisha kisiasa.
 

Nilikua anxious kusoma ulichoandika, umeandika vizuri ila mwishon ukakosa ustaarabu kwa kujeli mleta mada tena bila staha! Self discipline inasaidia sana kwenye maisha yetu haya, and you luck it mostly....!
 

Mleta mada hiyo ni akili ya kufundishwa hebu jaribu kuchamganya na yakwako acha upumbavu
 
Mkuu asante kwa kunijibia hata mimi nilitaka kumuuliza hayo uliyomuuliza Sokoinekafa miaka kibao leo hii baada ya Mzee wa watu kumsema baba Fred jamaa ndio anamkumbuka Moringe,tena akamsaidie huyo Fred kunywa viroba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…