Rogie
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 7,584
- 6,694
Washambuliaji Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka wafungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.
Kutokana na wachezaji hao kuibuka vinara kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga mabao 14, watagawana zawadi ya mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000.
Yanga imemaliza Ligi hiyo ikiwa bingwa kwa ponti 68 na kufunga jumla ya mabao 57, wakati Ruvu Shooting iliyomaliza katika nafasi ya saba kwa ponti 36 imepachika jumla ya mabao 28.
Watakabidhiwa zawadi hiyo katika hafla ya tuzo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 itakayofanyika kesho kutwa (Mei 24 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA