Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,200
- 10,947
Tangu jeshi la IDF liweke vifaru vyake pembezoni mwa Gaza ikitishia kuingia ndani ya Gaza kuwasaka Hamas,Iran imekuwa ikitoa maonyo makali kwa Israel isithubutu kufanya hivyo kwani itakuwa ni kuvuka mstari mwekundu katika mzozo huo ikiashiria na wao wataingilia kati kupambana kuwatetea wapalestina.
Tangu Ijumaa iliyopita jeshi hilo La IDf limetangaza kuvusha vifaru vyake kuingia Gaza. Ijapokuwa vifaru hivyo vimekuwa vikipata upinzani mkali na kulazimika kurudi nyuma kutoka kwa Hamas, hata hivyo ni kweli vimevuka mpaka na vimeuvuka huo mstari mwekundu uliochorwa na Iran.
Kinyume na kurudisha mapigo kwa kasi Iran imeendelea kutoa matamko ya kubembeleza na kulalamika na kuonya zaidi kwa kusema wao wameambiwa wasiingilie vita hivyo lakini mbona Marekani inazidi kuiunga mkono Israel.
Uungaji mkono huo wa Marekani na washirika wake hasa UK ni kweli upo na uko kwa maneno na vitendo.Bado tu Iran inaendelea kushuhudisha watu kuwa hao walioamrisha wakae kimya wanavunja makubaliano.
Muda huo huo Israel ikiwa imevuka mpaka na ndege zinadondosha mabomu ikiwemo aina mpya ya Iron sitng, nchi kama Saudia zina ratiba ya kukutana na viongozi wa Marekani wiki ijayo kuzungumzia masuala ya Gaza na uwezekano wa kusitisha vita. Inawezekana wanachokusudia kukizungumza sio kusitishwa vita bali wana ajenda nyengine tofauti .
Hayo yote yakitokea Gaza, kule ukanda wa magharibi na mashariki, kiongozi wa PLO ndio kabisa amepiga kimya kama kwamba ni mgonjwa huku walowezi wa kiyahudi wakiwaua wapalestina na kuwafukuza kwenye majumba na mashamba yoa.
Sambamba na walowezi jeshi la IDF limekuwa likipiga kutoka angani kama linavyofanya kule Gaza.
Kuhusu yanayowakuta wapalestina wa upande huo,raisi Biden ametoa tamko jepesi la kutaka walowezi waache kuwapiga wapalestina na upande wa Shinbet, shirika la ujasusi la Israel wametoa matamko kama hayo bila kutaka jeshi la IDF kuacha mashambulizi yake.
Kila mmoja kati ya wale walioonekana kuwa wangekuwa watetezi wakali na wenye sababu za kufanya hivyo kwa wapalestina katika muda ambapo misaada yao ni ya lazima, watakuwa wana sababu zao ambazo hawajaweza kuzidhihirisha.Kubwa linalofanana kwa wote ni kuhofia madaraka na mipango yao kwa hofu kuwa Marekani na Israel zitawapiga au zitawavunjia mipango yao hiyo.
Kwa mfano Saudia wana mradi wa kuigeuza nchi hiyo kuwa pepo ya dunia ambao wasingependa urudi nyuma na hasa kwa vile wameshatumia gharama kubwa sana mpaka hapo walipofika.Watu watasemaje ikiwa miradi hiyo haitokamilika.
Wakati watu wanakufa kwa njaa na kiu Gaza, Misri imetoa sababu za kilemavu za kutokufikisha misaada Gaza ikiilaumu Israel wakati kumbe mpaka wa Rafah wala haujapakana na Israel, ni baina yake na Gaza tu na pia upekuzi wa malori ya misaada hufanyika kilomita 62 ndani ya Misri kabla ya hata kufika huko Rafah.
Iran kwa upande wake iko karibu kukamilisha kurutubisha silaha zake za nyuklia na sijui zikikamilika wanakusudia kumpiga nani.
Kimya cha Mahmoud Abbas na viongozi wenzake wa PLO ni ahadi ya kumilikishwa Palestina pamoja na Gaza kitu ambacho baada ya Israel kufanikiwa kuikamata Gaza kama watafanikiwa wala hakitotekelezwa.
Maelezo na sababu ni kama hizo kwa Syria na Jordan.Kila mmoja akiwa na hofu ya kitu fulani alichonacho mkononi.
Kilichobaki ni Hamas wapigane kwa nafsi zao kwa silaha hafifu walizonazo wakitegemea msaada wa Allah mwenye nguvu za kweli na ambaye rehema zake huenea kote na huja wakati usiotegemewa.