ukiona bado hujalipuka ujue maumivu hayajafika sehemu yake.... yanaweza yakaja taratibu ukayapuuzia huku ukiyaweka kichwani lakini siku yakilipuka ndo utakapoona kila rangi.... huo ndo muda ninaoutumia hasa kuwa mwenyewe. na inanisaidia.
Unapoamua kujitenga ni vizuri ukawa unajua hasa nia yako ya kujitenga. Unaweza kujitenga kwa muda na ukapata solution nzuri sana kwa msongo wako kuliko kusikiliza huyu na yule wanasema nini. kuna ambao wanajiua pia kwa kusikiliza maneno ya watu, kila mtu anakuambia lake mpaka unajiona kama huna maana tena unaona ni bora uishie.
Nina miaka mingi sijalia, kweli ukiona yatima ana ndevu basi moyo una mvi.
Maumivu yanayosababisha msongo wa mawazo mara nyingi huwa ni mauzmivu ya muda mrefu, wakati mwingine ni kitu kinachotokea kwa mchakato wa taratubu hata inakuwa ngumu kugundua kuwa kinakuletea msongo.
Sasa sijui utajitengaje na watu ili upate wasaa wa kulia. Unapokuwa natatizo lazima kuna muda ule wa mwenyewe kutafakari na kuumia kabla hujakata shauri la kushirikisha watu au kufanya maamuzi.
Watu wengi wanajiua huwa wanakuwa na dalili za kujitenga, ndio maana unapokuwa na msongo wa mawaza unashauriwa kukaa na watu. Ni hatari kuwa na msongo mkali afu ukakaa peke yako.
hii huwa naipenda sana. Inanisaidia kujitafakari....
Huwa kitu cha kwanza kukifanya ni kujifungia na kulia sana, yaani nalia mpaka nione nimetosheka......
Ninapomaliza hapo huwa naanza kutafakari kilichotokea, naweka issue kwenye angle zooteee. najaribu kujiweka kwenye shoes za aliyenitenda, kama ningekuwa mimi ningefanya hivyo? namuhukumu na kumtetea mimi mwenyewe. Nikijiridhisha naanza kusali, kwenye process nampa msamaha (ndani ya moyo wangu). Nikishamsamehe nakutana naye kumtaarifu nimemsamehe na kujadili the way forward (kuendelea au kummwaga).
Nilishapatwa na hii kitu, na ilikuwa ngumu. Niliondoka nyumbani, nikaenda kwa dada na nikawa mtu wa kukaa ndani tu. Nilikuwa nasoma kila kitabu, jarida au kitu chochote kilicho mbele yangu kama njia ya kujidistruct.
Ilibaki nusura niolewe na mtu just for the sake of it, namshukuri dada aliniokoa tena na hilo.
Recently yakipandana sana kichwani, naishia kusali tu (kufunga, novena etc). Anyway, mimi sio mtu sana wa kuyatoa kwa mtu mwingine yale yanayonisumbua hasa, nikishare ni ya juu juu tu na mostly kwa ajili ya kumfanya mtu aone namtegemea. So l think nikiacha kusali, au nisingekuwa na mtoto ninayempenda sana, huenda nami ningekuwa candidate wa suicide.
kwa aliewahi kupitia msongo wa mawazo wengi wao hutulizwa kwa kushirikisha watu, mie ni mmoja wapo, ningekaaga kimya ningedata kabisaaa, ukiwa na watu wazuri watakushauri vizuri na hiyo hali huisha kabisa.
rafiki, believe me usingejiua.....
wangapi wanajiua na wana watoto na vitu vingine vingi tu ambavyo wanavipenda.
wewe hiyo ndo style yako ya ku-deal na msongo wa mawazo. kama hapo juu nilivyosema, kila mtu ana style yake, na inamsaidia. Mimi pia natumia sana hiyo ya kujifungia, kusali na kujitafakari, na hata siku moja sijawahi jiwa na wazo la suicide.
Mie namshukuru Mungu sana hii kitu sijakutana nayo. Muziki kwa upande wangu husaidia sana katika kuepukana na hali hii. Namuomba Muumba wetu hali iendelee kuwa hivi maana hii kitu ni hatari sana.
…..Kiukweli humu maishani watu tumegawanyika kutokana na jamii, koo na familia tofauti tofauti
#factor ambayo kwa kiwango kikubwa inachangia hali ya mtu kukabiliana na Usongo wa Mawazo.
Kuna familia ambazo #MtotoWaKiume anakuzwa akijijua yeye ndie tegemeo la familia, kiasi kwamba
mafanikio yake kimaisha au anguko lake la kimaisha linaathiri moja kwa moja familia yake.
Akikoswa koswa na Wazazi, basi Mkewe, Wakweze na wanawe wanamtazama kwa jicho la "huyu naye Loser tu,…!"
Kuna familia mbazo haijalishi ni mtoto wa kike au wa kiume, lakini kwakuwa wazazi wana high expectations na
mtoto wao huyo, mafanikio yake au anguko lake pia linaathari kwake na familia nzima.
Hivyo hivyo katika maisha ya mahusiano, ndoa na Urafiki. Wengi wetu tunajikuta tunapoamua kuingia katika mahusiano Matarajio ya jamii, familia na wengi wanaotuzunguka ni kwamba Kudumu au kuvunjika kwa mahusiano husika yana athari kwao.
Hizi High Expectations ndizo zinazopelekea wengi wetu kukumbwa na huu Usongo wa mawazo. Kwa Upande mmoja, tunataka tuwe In-Control na maamuzi ya maisha na furaha zetu,…kwa upande mwingine, ile pressure ya 'kuwafurahisha' wanaotuzunguka nayo inatukabili left-right and centre….
Ni rahisi kumwambia mtu, 'ukitaka kukosa furaha maishani, ishi kwa kufurahisha watu'….
Hivi kuna mtu ambaye hapendi kuwa appreciated jamani?
Mambo haya kwa mtazamo wangu huwapelekea wengi wanaokumbwa na Usongo wa Mawazo kuamua kufanya maamuzi kinyume na matarajio ya wengi….au kwa maana nyingine Self-Destructions huanzia hapo na maswali lukuki mfano;
- nini thamani ya utu wake?
- kwanini kapoteza mudawake?
- kuna faida gani baada ya yaliyotokea?
Je? Matukio ya vijana kufanya mauaji sababu ya kujihisi hawapewi Appreciation 'stahiki' ni kwakuwa sisi #Generation mpya ya wazazi tunayafumbia macho yale ya msingi katika Mahusiano na yanayopelekea Usongo wa Mawazo…..?
…na tuendelee na mjadala
Cc Fixed Point Mentor Kongosho Tuko Mapi Kaunga Nyamayao,….na wengineo mliobobea katika kuchangia 'mada nzito'
safi sana, .!
Maana inakubalika, "You can't Control what you feel, But you can control what you think!"
kwa kitendo cha kujipa muda ina maana umeweza jijengea 'Delaying' tactics za maana
sawa na wale wanaosema 'fikiri kabla ya kutenda' badala ya 'kutenda kabla ya kufikiri'
Naamini kwa wanaotaka kujifunza zaidi toka kwako, watataka kujua umewezaje mpaka
ukafanikiwa kui train [Tame!] akili yako mpaka wewe ukawa unaiongoza akili yako 'badala akili kukuongoza.'
Big Up Bro.
nimependa ulivyoandika ni kama umeandika kwa niaba yangu kama umenisoma yaani!hii huwa naipenda sana. Inanisaidia kujitafakari....
Huwa kitu cha kwanza kukifanya ni kujifungia na kulia sana, yaani nalia mpaka nione nimetosheka......
Ninapomaliza hapo huwa naanza kutafakari kilichotokea, naweka issue kwenye angle zooteee. najaribu kujiweka kwenye shoes za aliyenitenda, kama ningekuwa mimi ningefanya hivyo? namuhukumu na kumtetea mimi mwenyewe. Nikijiridhisha naanza kusali, kwenye process nampa msamaha (ndani ya moyo wangu). Nikishamsamehe nakutana naye kumtaarifu nimemsamehe na kujadili the way forward (kuendelea au kummwaga).
kulia ni njia mojawapo ya kujiondolea emotional overload na kupunguza hasira!Unalia umekuwa mtoto?
kulia ni njia mojawapo ya kujiondolea emotional overload na kupunguza hasira!
Kuna mambo mengine makubwa sana but principles zake ndoogo sana. Mfano mi naamini watu wanaoathiriwa sana kukosa appreciation ni wale wanaokuwa na over-expections kutoka kwa wengine...
Sometimes tunawaamini watu sana kutokana na wanayoongea, tukasahau kuwa binadamu anaishi less than 20% ya anachowaza na kuongea. Hata uwe unamwamini mtu namna gani, as long as ni binadamu tegemea kuna siku atakufanyia kitu cha kipuuzi tu, na asipokufanyia, basi ni kwa bahati tu...
Labda niseme inategemea na hatua ya msongo.
Ukiona unaweza kusolve msongo wako peke yako basi msongo huo bado ni managebale, kuna misongo mingine inarusha akili kule, mtu anakuwa mgonjwa kabisa, hali, halali, haongei. Ni kama vile mtu anatamani ku-resign kuishi, bila msaada ni ngumu sana.
Hata hivyo, nakubaliana na kuwa watu tunatofautiana strength ya kukabiliana na dhamama, wengine shock up zao za bajaj, wapo pia wenye shock up za samtrela.
Mie naamini asilimia kubwa tunapitia misongo ya mawazo, labda tujiulize misongo hii inafikia hatua gani? Mwisho wa siku nakubaliana kuwa binadamu japo tunafanana sana, ila tunatofautiana sana hasa kihisia na uwezo wetu wa kubeba mambo.
Uko sawa, huenda kweli ni level au stages za depressions zachangia watu wengine kufikia kujiua. Nimesikia story nyingi za wababa kujiua baada ya madeni au kudhulumiwa kibiashara, vijana kujiua baada ya kufeli mitihani, watu kujiua baada ya majibu ya HIV status etc.
Kuongea au kuchangamana na watu kwasaidia emotionally lkn pia kunasaidia watu kukumonitor usipate nafasi ya kujidhuru; lkn kwetu wengine ambao hukimbilia ibada nayo yafanya kazi tena zaidi kwani unagundua tatizo ni la muda tu na pengine sio kubwa kihivyo kama ambavyo shetani anakudanganya. Believe me it helps a lot more. Imagine unamwambia mtu mwenye uwezo wa kuliondoa hilo tatizo au hata kulifanya liwe jepesi kama mifuko ya hewa badala ya misumari; tofauti na shoga ambaye the best she can do ni kukupa a shoulder to cry on.
Mbu over expectations ni tatizo kubwa, na maoni yangu kama mzazi ni kumfanya mwanangu ajue "it is okay to make a mistake or two" na kwamba failure is a learning process na sio doom. Personally nilishaacha kujali ndugu au jamii inategemea nini toka kwangu, ninafanya kile ninachoona right.