Msomi ni nani?

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
351
866
MSOMI NI NANI AU NI MTU WA NAMNA GANI

Na: Comred Mbwana Allyamtu.


Hivi karibuni nilikuwa na mjadala mzito na na makomled wenzangu kuhusiana na dhana nzima ya mtu kujiita kuwa ni msomi.Chan zo cha mjadala huo ilikuwa ni pale nilipo waeleza kuwa kuna mahali siku ya leo nimealikwa katika meza ya mjadala juu ya mada ya "Msomi ni nani? Au ni mtu gani? Wakati tukiendele kulizungumzia hilo ndipo Comred mwenzangu aliponitaka niachane na biashara niliyoianzisha ili niendelee na elimu ya juu, kwani hapendi kuniona nikibobea katika biashara na binadamu bota ni yule ambaye ni msomi. Basi hapo ndipo nilipoanzisha mjadala wa kutaka kujua kwamba *msomi* ni mtu wa namna *gani*? Au je mtu anaweza kupimwa kwa vigezo gani ili aitwe kuwa ni *msomi*?

Mjadala huo ulikuwa ni mzito na uliochangamsha pale ofisini kwangu kwani kila mtu alipata nafasi ya kuchangia kwa mtazamo wake, na kutokana na mjadala huo nimejifunza mambo mengi sana kuhusiana na hii dhana ya mtu kuitwa kuwa ni *msomi*.

Hebu niwaulize wasomaji wa kwenye group hili na wanablog wenzangu, hivi *msomi* ni nani? Kama mtu amesomea taaluma fulani labda tuseme, udaktari, uhandisi au udaktari wa falsafa, Je huyu anaweza kujiita kuwa ni *msomi*?

Nimeuliza hivyo kwa sababu kama mtu ni *msomi* kwa maana ya dhana ya usomi tunayoifahamu, basi atakuwa anajua kile alichofundishwa na kukaririshwa tu akiwa darasani, lakini yeye mwenyewe hajawahi kuwa na kitu chochote kipya alichobuni.

Kama ni hivyo basi sioni kama kuna mtu anayeweza kujivuna kuwa yeye ni msomi.Atajiitaje kuwa ni msomi wakati amekaririshwa nadharia za wengine pasipo kubuni kitu chake mwenyewe?Nadhani hiyo inatosha kuvunja dhana ya watu kujiita wasomi.

Hivi ni nini tofauti kati ya msomi na yule ambaye hakuwahi kuingia darasani hata siku moja?

Kwangu mimi tofauti iliyopo labda ni kwamba, mmoja ametembea sana kutoka nyumbani hadi darasani na mwingine hajawahi kufanya hivyo hata siku moja. Huyu aliyetembea sana kwenda darasani kutafua elimu, amevuliwa akili yake na kupewa akili ambayo ni nadharia za watu wengine, zikiwemo zile sahihi na zisizofaa hata kuzitazama. Lakini amezikubali hizo nadharia na hivyo anaitwa kuwa ni msomi.

Kwa mfano ukienda chuo kikuu unafundishwa hata namna ya kulitazama jambo na kulihukumu kwa kutumia akili za watu wengine. Kile ulichokuja nacho, yaani imani na ufahamu wako kuhusu maisha, uchumi na siasa vinaondolewa na kuwekewa ambacho unatakiwa ukiamini na kukitetea kwa nguvu zako zote bila kuhoji, na hiyo itakufanya uitwe labda daktari wa falsafa na kutunukiwa digrii yako ya tatu, na kuanzia hapo utaitwa msomi!

Kumbuka kwamba digrii ni karatasi zaidi kuliko maarifa, ndio maana dunia nzima inasumbuliwa na wimbi la digrii feki.Ninachojua mimi ni kwamba wasomi wengi wa vyuo vikuu na madigrii yao ni wajinga sana kwenye maeneo mengine ya maisha.

Na jambo lingine ambalo linanishangaza, ni dunia hii kuendelea kukumbatia karatasi kama kipimo cha usomi. Unaweza kukuta mtu hajui chochote, lakini kwa sababu ana makaratasi yake yanayosema amesomea Shahada ya Uchumi, basi atapewa nafasi kubwa. Kisa ni karatasi!Halafu baadae mnashangaa, kwa sababu hana anachozalisha.Sasa usomi ni kitu gani, ni karatasi, ni kukariri nadharia za watu wengine, ni kujua jambo kwa undani au ni kujiuliza na kutafuta jibu?

Kuna watu wengi ambao nawafahamu, ambao wamekariri sana elimu ya darasani, wanayo madigrii lakini ukizungumza nao, utafikiri umekutana na mtu ambaye hajawahi kutia mguu darasani hata siku moja. Na wangine wako mitaani hawana kitu,na wamekata tamaa na maisha, kisa hakuna ajira.

Kwa kuamini kwamba karatasi ndizo zinazomfanya mtu kuwa msomi ndio maana sisi vijana wengi huko mashuleni na vyuoni tunajitahidi kushindana kukariri ili tufaulu sana na kupata digrii za viwango vya juu.Tunachotaka ni karatasi ili tupate ajira na wala sio maarifa. Tunapomaliza masomo tunatoka kama tulivyoingia na pengine tukiwa tumechuja zaidi kiufahamu.

Nimewahi kujiuliza swali hili, hivi watu kama Arstotle Sophocles, na baba wa elimu dunia kama Socrate na wale wajuzii wa kwanza kwanza duniani, walifundishwa na nani, walikaa darasa lipi na kupewa vyeti gani? Hadithi za kale utuambia kuwa mgunduzi wa Meli Arichimidis hakuwai kwenda dalasani kabisa lakin nadharia yake huishi mpaka leo na nizaidi ya miaka 1700 iliyopita. Lakini kuna watu kama Galileo Galilaya, Hopecus pia awajilui kabisa kitu kinachoitwa "kukaa dalasani".

Mwasisi wa somo la dhana ya falsafa ya sayansi ya historia duniani *Hipecus* na mwasisi wa dhana ya daktali duniani Hipocratus ni nani aliowafundisha? Kama msomi shariti lake lazima ukae dalasani?
Hawa hawakukaa darasani, bali walizalisha maarifa baada ya tafakari kubwa na ya muda mrefu. Walijiuliza maswali ili kupata majibu, waweze kuisaidia jamii hapa duniani.

Kwa mtazamo wangu hawa ndio wasomi, kwa sababu utafiti wao unagusa kila eneo la maarifa bila kujali kama ni sayansi, biashara, tiba au sanaa. Kwa mantiki hii msomi sio mtu mwenye makaratasi bali msomi ni mbobezi wa kujiuliza maswali na kutafuta ufumbuzi juu ya maswali yake. Lazima msomi awe na matokeo chanya katika jamii juu ya maarifa yake binafsi sio maarifa ya kukarilishwa kutoka kwenye nadharia za watu ambao ndio walikuwa wasomi.
Msomi ni mtu aliye huru kutafuta maswali kuhusu maisha yetu.

Mtawala wa kwanza wa Dola ya Rumi (Rome Empire) Jurius Kaisal alipo lihutubia Balaza la Seneti (COUNCULIS SENETI) lake la kwanza kabisa alilo buni kama njia ya kurahisisha utawala kwa watu wake karne ya 15th BCE alisema
"Maarifa ni zao la akili linalotokana na ubunifu wa mawazo ambayo mtu ujiuliza kwa kina na kutafuta ufubuzi yakinifu na kisha kutoa matokeo yatakao ishangaza jamii na kimsingi huyu ndio msomi" lengo langu sio kueleza habari za huyu bwana ila nimejalibu kuweka nukuu hii ili tuweze kumjua *msomi* ni nani?

Sasa DUNIA imekuwa na watu kibao wanaojiita wasomi lakini ndio hao awawezi hata kujipambanua katika yale yanayo wasibu katika mazingira yanayowazunguka. Nakumbukahawa hawa tunao waita *wasomi* ndio hawa waliotufikisha hapa kwenye wimbi la ufisadi, urafi wa mali za wanyonge, ukadamizaji wa haki za binadamu, ubinafsi, ubaguzi wa rangi, kutetea ushoga, uongo uliokithili, na uchonganishi baina ya binadamu, katika uso wa DUNIA hii lakini bado wameendelea kuitwa eti wasomi sababu wanamiliki mafaili ya makaratasi ya vyeti.

Ndimi
Comred Mbwana Allyamtu

+255765026057
+255679555526
Mbwanaallyamtu990@gmail. Com
 
Back
Top Bottom