Msomi anapokuwa mwanasiasa

Ni mweli usemayo MwanaHabari ila kama unasoma vizuri sidhani kama kuna sehemu amesema wajinga ndo wawe wanasiasa! Si amesema wanasiasa wanatakiwa wajiendeleze kimasomo no?

Nafikiri mwandishi amelisema /andika hili kwa kuwa ameona kasi ya wasomi kukimbilia kwenye siasa imekuwa kubwa kiasi cha kutishia profession hii. Mimi nafikiri wasomi wetu wangebaki kuwa wasomi ili waweze kuwakosoa wanasiasa wetu pale wanapokosea after all hilo ndilo jukumu lao kwa wananchi apart from lile la kutusomesha baadhi yetu au? Maana msomi akiwa mwanasiasa atakosolewa na nani?
 
Inawezekana wanaingia kwenye siasa kwa kujiunga na makundi yenye maslahi tofauti katika siasa za TZ. Mi naona wengi wameamua kutofanya wanachotakiwa kufanya, badala yake wanalinda maslahi ya kambi walizojiunga nazo wakati wanaingia kwenye siasa.Sidhani wasomi wotee wamepoteza vichwa vyao vya kisomi kwa ajiri ya siasa.
 
Ni mweli usemayo MwanaHabari ila kama unasoma vizuri sidhani kama kuna sehemu amesema wajinga ndo wawe wanasiasa! ''''''''''''''
'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''' kasi ya wasomi kukimbilia kwenye siasa imekuwa kubwa kiasi cha kutishia profession hii.

MWANAJIMIIONE,
Mawazo yako ni ya kijamii hasa.
Kwa hapo, tuko pamoja mkuu.
 
Unapoingia kwenye siasa huwezi kuwa na mawazo independent kwa maana kuna miongozo, sera, ilani na mfumo ambao uko established.Msomi mwenye kustahili kuitwa msomi anatakiwa awe na mawazo yake na kuwa tayari kwa paradigm shift kutegemeana na anaamini nini ( conviction).Ili u survive as a politiciam inabidi uwe tayari kutelekeza fikra huru na kuungana na wenzio - CO-OPTATION!
IF U CANT BEAT THEM, JOIN THEM.

WOS,
Here you are.
Siasa humlazimisha mtu kuishi mawazo ya wengine na kukumbatia itikadi ya chama hata kama ni uozo,.
Kweli SIASA SI HASA.
 
WS nakubaliana na wewe kuhusu ugumu wa mwanasiasa kuwa na thought zake binafsi. Lakini nimjibu kwanza Exaudi Makyao kwamba tatizo letu tunaloliona katika siasa kama kubwa lipo pia katika fani nyingine zote.

Walimu, wahandizi, matabibu, viongozi, wafanyabiashara, viongozi wa dini na wataalam kwa wingi wao wamekosa kitu kimoja muhimu sana. Nacho ni UZALENDO. Uzalendo huu wameukosa kutokana na mfumo wetu wa elimu kuwa wa kunakiliwa kutoka kwenye ule mtaala wa wakoloni. Hakuna vionjo vya kumfanya mtu anayepata elimu ya Tanzania aipende Tanzania hata kidogo. Zaidi kila aipataye anaichukia nchi yake.

Ufisadi, rushwa ubadhirifu, umangimeza na ukiritimba vinawakuta wale tu wasio na mapenzi kwa nchi na watu wake.

Ili tuondoe tatizo hili ni lazima tubadili ndani nje mfumo mzima wa elimu. Elimu izalishe wapenda nchi ambao hawawezi kuisaliti nchi na watakaopambana na kila adui wa nchi wa nchi kama ilivyo kwa waisraeli, USA, Venezuela, Cuba, na nchi zote za Ulaya Magharibi..
 
Jambo la kwanza ni tafsiri fasaha na halisi ya msomi na mwanasiasa. Je msomi ni mtu mwenye PhD? .... Ni vigezo gani tunavitumia kumuita huyu msomi na huyu si msomi?

Na mwanasiasa ni nani? Kuna msitari gani unaweza kuuchora kati ya mwanasiasa na msomi kiasi kwamba mmoja akitoka huku na kuelekea kule unasema amevuka msitari wake? Hili naliona gumu.

Siasa ni kitu kinamgusa kila mtu na unaweza sema kila mmoja ni mwanasiasa. suala linakuja tu ni mwanasiasa katika level gani? Ya uongozi? Mara nyingi tunawaangalia viongozi peke yao kama ndo wanasiasa. Lakini ikiwa hata sisi tunachokifanya hapa kinaweza kutafsiriwa kama siasa basi tu wanasiasa ati.

Ikiwa ni vigumu kusema hii ndo tafsiri ya usomi na hii ndo tafsiri ya uanasiasa basi pasi na shaka yeyote anaweza kufanya chochote.

Usomi; Je usomi maana yake ni profesionalism? Profesionalism ni utaalam. Je utaalam na siasa hiviingiliani? Siasa hazihitaji utaalam au utaalam hauhitaji siasa? Ikiwa siasa zinahitaji utaalam na utaalam unahitaji siasa basi kuna kosa gani kwa mwanasiasa kuwa mtaalam, au kuna kosa gani ikiwa mtaalam anakuwa mwanasiasa?

Hakuna kosa hata kidogo! Siasa zinahitaji utaalam. Na hata utaalam unahitaji siasa vile vile. Unless tunataka siasa zisizo na mwelekeo au utaalam usio na mpangilio au mpango.
 
Siasa mara nyingi ni kufanya mambo kwa kuangalia maoni ya umma; iwe ni biashara au shughuli yoyote ya kitaalam. Siasa zinazozingatia utaalam hasa ndo siasa muafaka zinazoleta maendeleo kwa umma husika. Utaalam vile vile ukifanywa na kutekelezwa kuzingatia maoni ya umma tunaweza kusema huo utaalam unafikia malengo yake vilivyo. Ikiwa hivi ndivyo basi siasa na utaalam vinategemeana na vinakamilishana na hivyo vinahitajiana. Usomi unahitaji siasa ili kuupa tafsiri na maana kwa umma unaohusika wakati Wakati siasa zinahitaji usomi au utaalam ili kuzipa mwelekeo unaoleta maana kwa jamii badala ya kuwa chanzo cha migogoro na mikinzano tuu.
 
............................... Kuna msitari gani unaweza kuuchora kati ya mwanasiasa na msomi kiasi kwamba mmoja akitoka huku na kuelekea kule unasema amevuka msitari wake?....................................

.

KIPIMAPEMBE,
Mkuu nakuheshimu,
Mchango wako umekaa kifalsafa sana.
Labda lile jukwaa la Falsafa likianzishwa, tutafurahia sana falsafa zako.

Hata hivyo,
Ukweli unabaki kuwa wengi wa wanaojihusisha na majukwaa ya siasa sasa hivi, hawafanyin maamuzi kulingana na kanuni za Taaluma walizosomea,
Badala yake wamebaki kulinda itikadi fulani tu.
 
Sawa EM,

Lakini tukubaliane vile vile kuwa vile tunavyoendesha siasa zetu kuwa si ambavyo siasa inatakiwa ziendeshwe. Kwanza hizo itikadi katika siasa zetu mi sizioni kabisa. Kilichopo ni ushabiki, kama Simba na Yanga. Angalau kungekuwwa na itikadi nafasi ya utaalam ingeonekana.

Ikiwa wataalam wetu kwenye siasa wanafanya maamuzi kiushabiki zaidi, tukubaliane kuwa si jinsi siasa zinavyoendeshwa sehemu nyingine yoyote penye siasa za kistaarab na kimaendeleo.

Tukubali basi kuwa wasomi wetu katika siasa wanafanya hivyo si kwa sababu hivi vitu haviingiliani, bali kwa sababu tunaendesha siasa zetu kibabaishaji mno. Vinginevyo bado nafasi ya mambo kwenda kitaalam ndani ya siasa ipo na ndio tunachotaraji wote kitokee.
 
Mtazamo wangu, tukiacha falsafa nyingi ambazo zitatuchanganya bure, hebu chukulia mfano rahisi kama wa Prof Sarungi, hamfikiri kwamba kwa yeye kuwa MOI anaweza kuwa tija zaidi kuliko kuwa mbunge wa Rorya?

Msolla anatoka SUA anakwenda kuwa mbunge... bado Luhanga, yeye sijui nae akawe mbunge wa wapi!!!

Wanasiasa wasomi wapo na waliofanyika msaada bungeni tumewaona, lakni kama alivyotangulia kusema mmoja wenu hapa, vyama huongozwa na itikadi. Swali ni kwamba wanaondaa itikadi/sera za vyama vyao, je huwa ni wasomi? Shauri yenu, ndio hapa wazee wanakaa wanaweka mahakama ya kadhi kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, kimbembe kinakuja kui deliver hiyo ahadi....
 
:eek:
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?

THERE IS POLITICAL SCIENCE AMBAYO INAWASOMI...KWA HIYO WANASIASA WANATAKIWA KUWA WASOMI HASA....
 
:eek:

THERE IS POLITICAL SCIENCE AMBAYO INAWASOMI...KWA HIYO WANASIASA WANATAKIWA KUWA WASOMI HASA....

SAWA mkuu,
Lakini kwanini wasomi wengi wanapoingia katika siasa huacha kutumia kanuni za utaalamu wao katika kufanya maamuzi?
 
Kwa mtazamo wangu, wataalamu wetu wasomi wanapoingia katika siasa huwa wanasahau kanuni na miongozo ya Elimu yao.
Wengi hujikuta hawaelewiki tena kama na wataalamu wasomi.
Hata wakiandaa kwa mfano, bajeti za nchi, huziweka katika sura ya kisiasa.Tutafanikiwa kwa mwenendo huu kweli?

Wasomi wengi wapandeo kujiingiza kwenye siasa, hususan Tz, inabidi uwaangalie mara mbilimbili kwani usomi wao mara nyingi aidha ni wa kukremu (yaani wazuri wa nadharia ya kuhamisha vitabu vichwani mwao, na siyo utumiaji wa hiyo nadharia kwenye maisha ya kila siku) tu, au kuna aina fulani ya ukihiyo kwenye historia ya maisha au masomo yao
 
Wasomi wengi wapandeo kujiingiza kwenye siasa, hususan Tz, inabidi uwaangalie mara mbilimbili kwani usomi wao mara nyingi aidha ni wa kukremu (yaani wazuri wa nadharia ya kuhamisha vitabu vichwani mwao, na siyo utumiaji wa hiyo nadharia kwenye maisha ya kila siku) tu, au kuna aina fulani ya ukihiyo kwenye historia ya maisha au masomo yao

Nakubali mkuu.
 
Sasa ndio wakti wa wasomi na vijana kuingia katika siasa na kuchana na vizee vilivyo stahafu kazi kisha kuja kwenye siasa. hawa ndio wale wanaolala Bungeni.
 
Sasa ndio wakti wa wasomi na vijana kuingia katika siasa na kuchana na vizee vilivyo stahafu kazi kisha kuja kwenye siasa. hawa ndio wale wanaolala Bungeni.

Umesikika mkuu.
Ni panya yupi yuko tayari kumfunga paka kengele?
 
Mkuu hapo nakubaliana nawe.Tunao wasomi kibao ambao ni "watukuka" katika taaluma zao lakini toka waingie ndani ya siasa(si-hasa) wamekuwa ndivyo sivyo!Kwa maoni yangu watu wangejikita katika taaluma zao hata kama hazilipi haraka kama siasa ambayo baadaye huwadhalilisha sana.
Mfano Prof.Sarungi kafikia hatua ya kudhalilishana na wapinzani wake kule Rorya,aibu iliyoje!
 
Back
Top Bottom