Ndege Tausi
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 992
- 472
Niliwahi kuleta hoja yangu kuhusu msitu huo ambao upo wilayani Kasulu lakini sijui kwanini hoja hiyo haikuchapishwa. Sielewi msimamo wa serikali kuhusiana na msitu huo ambao unaendelea kuharibiwa. Msitu huo umevamiwa na watu kutoka sehemu mbalimbali na wengine kutoka nje ya nchi wanaendelea na shughuli zao kwa raha zao bila kubughudhiwa. Serikali ipo kimya na serikali za vijiji vinavyouzunguka huo msitu havina uwezo wa kuchukua hatua yoyote. Hofu yangu ni kuwa msitu huo utaendelea kuharibiwa kutokana na watu kuendelea kuingia kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo wafugaji waliofukuzwa kutoka mkoa wa Kagera. Tatizo hili ni la muda mrefu kama miaka 8 hivi.
Tunaomba serikali ya mkoa pamoja na serikali kuu washughulikie tatizo hili kwani sisi wenyeji wa mkoa huu tunaona uchungu sana.
Naomba serikali na yeyote yule mwenye majibu juu ya tatizo hili atoe ufafanuzi kama tatizo hili litashughulikiwa lini?