Msiogope kudai zawadi mlizopeana wakati wa uchumba, penzi likiwa la moto. Sheria ipo na inafanya kazi

Red black

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2019
Posts
11,858
Reaction score
36,543
Wakuu msiogope kudai zawadi zenu mnazopeana wakati wa uchumba/penzi likiwa moto kwa ahadi ya ndoa ikiwa mahusiano hayo yatavunjika.

Sheria ipo na inaifanya kazi.

Ukweli ulivyo

Sheria ya Tanzania inatambua kuwa unapoingia kwenye uchumba, unakuwa umetoa ahadi ya kisheria ya kuja kufunga ndoa. Sasa, ikitokea mmeachana Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inaruhusu mmoja wenu kwenda mahakamani kudai kurejeshewa zawadi alizozitoa kwa mwenzake.

Lakini hapa kuna siri moja kubwa ambayo watu wengi hawaielewi: mahakama hairudishi kila kitu. Zawadi ndogo ndogo ambazo wapendanao hupeana kila siku kama ishara ya upendo kwa mfano hela ya kusuka, vocha, gharama za mitoko, au nguo za kawaida, hizo huwezi kuzidai kwa sababu zinahesabika kama sehemu ya mahusiano ya kawaida ya watu wanaopendana.

Sheria inatazama zaidi zile zawadi kubwa na za kudumu ambazo mlizitoa kwa lengo mahususi la maandalizi ya ndoa yenyewe, kama vile pete ya gharama ya uchumba, kiwanja, gari, au vifaa vya ndani vilivyolipiwa kwa ajili ya nyumba mtakayofikia mkishaoana.

Pia, mahakama huangalia sana nani amesababisha huo uchumba uvunjike na kwa mazingira gani.

Ikiwa mwanamume ndiye amemwacha mwanamke bila kosa lolote la msingi (labda tu amepata mwingine), anaweza akashindwa kupata haki ya kudai zawadi alizozitoa kwa sababu yeye ndiye amevunja "mkataba." Sheria ina kanuni inayosema huwezi kufaidika na kosa lako mwenyewe.

Kwa kifupi, sheria hii ipo kwa ajili ya kumtetea yule aliyewekeza kitu chake kwa uaminifu halafu akaishia kuumizwa au kuachwa kinyume na makubaliano.

Muhimu ni kuhakikisha kuwa unapodai, unao ushahidi wa kutosha kuwa kulikuwa na ahadi rasmi ya ndoa (kama vile kuvishana pete mbele ya watu au kutambulishana kwa wazazi) na kwamba hiyo zawadi uliyotoa ilikuwa ni kwa ajili ya hiyo safari ya ndoa na siyo zawadi za kawaida za "hongera kwa birthday."

Screenshot_20260326-120505~2.jpg
 
Ikiwa km mliandikishiana kwamba uchumba ukivunjika anarudisha km hamjaandikishiana na ikagongwa muhuri na Mwanasheria au Hakimu au Jaji hapo hesabu umeliwa mkeka umechanika.
mkeka hauwez kuuliwa sheria ipo na inaifanya kazi
 
Sheria inasema muwe mmeandikishiana kwa Mwanasheria akagonga muhuri na akasaini sio uchumba tu hata ndoa mnaweza kufanya hivyo kwa kufuata taratibu za kisheria unapompa mchumba wako let say gari au nyumba

Kabla ya kumuoa au kuolewa nae unatakiwa usimpe km malikauli yaan lazima iende na documents za kusainishana na mashahidi na Mwanasheria akiwepo Mwanasheria anasaini wewe unasaini na Mashahidi wanasaini kabisa kwamba huu uchumba ukivunjika basi hii gari au nyumba unarudisha sio hivyo tu sheria inaenda mbali

Hata ukitaka kumsomesha mchumba wako wanasema mchumba asomeshwi ila ukifuata taratibu za kisheria mchumba anasomeshwa ila tu inabidi ufuate sheria yaan kabla ya lazima msainishane kabisa kwamba likitokea la kutokea ukavunja uchumba basi utalipa gharama zote nilizogharamika kwa ajili yako kipindi unasoma

Ushaelewa hivyo ndivyo sheria inavyotaka sio unakaa nae chobingo unampa gari then baadae anakukataa unajifanya unataka gari na wakati umesajiri kwa jina lake unategemea atakupa km sio kwamba umeshaliwa

Kwa hio lazima Mwanasheria ahusike yaan lazima agonge muhuri na asaini akikutapeli huyo mwanamke na umempa gari umempa nyumba peleka mahakamani fungua kesi atarudisha vyote
 
Wakuu msiogope kudai zawadi zenu mnazopeana wakati wa uchumba/penzi likiwa moto kwa ahadi ya ndoa ikiwa mahusiano hayo yatavunjika.

Sheria ipo na inaifanya kazi.

Ukweli ulivyo

Sheria ya Tanzania inatambua kuwa unapoingia kwenye uchumba, unakuwa umetoa ahadi ya kisheria ya kuja kufunga ndoa. Sasa, ikitokea mmeachana Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inaruhusu mmoja wenu kwenda mahakamani kudai kurejeshewa zawadi alizozitoa kwa mwenzake.

Lakini hapa kuna siri moja kubwa ambayo watu wengi hawaielewi: mahakama hairudishi kila kitu. Zawadi ndogo ndogo ambazo wapendanao hupeana kila siku kama ishara ya upendo kwa mfano hela ya kusuka, vocha, gharama za mitoko, au nguo za kawaida, hizo huwezi kuzidai kwa sababu zinahesabika kama sehemu ya mahusiano ya kawaida ya watu wanaopendana.

Sheria inatazama zaidi zile zawadi kubwa na za kudumu ambazo mlizitoa kwa lengo mahususi la maandalizi ya ndoa yenyewe, kama vile pete ya gharama ya uchumba, kiwanja, gari, au vifaa vya ndani vilivyolipiwa kwa ajili ya nyumba mtakayofikia mkishaoana.

Pia, mahakama huangalia sana nani amesababisha huo uchumba uvunjike na kwa mazingira gani.

Ikiwa mwanamume ndiye amemwacha mwanamke bila kosa lolote la msingi (labda tu amepata mwingine), anaweza akashindwa kupata haki ya kudai zawadi alizozitoa kwa sababu yeye ndiye amevunja "mkataba." Sheria ina kanuni inayosema huwezi kufaidika na kosa lako mwenyewe.

Kwa kifupi, sheria hii ipo kwa ajili ya kumtetea yule aliyewekeza kitu chake kwa uaminifu halafu akaishia kuumizwa au kuachwa kinyume na makubaliano.

Muhimu ni kuhakikisha kuwa unapodai, unao ushahidi wa kutosha kuwa kulikuwa na ahadi rasmi ya ndoa (kama vile kuvishana pete mbele ya watu au kutambulishana kwa wazazi) na kwamba hiyo zawadi uliyotoa ilikuwa ni kwa ajili ya hiyo safari ya ndoa na siyo zawadi za kawaida za "hongera kwa birthday."

View attachment 3562923
Vipi wale waliosomesha mademu zao na kujenga kwao kama zawadi ya uchumba na mihadi ya kuoana sheria inawaweka upande gani..
 
Back
Top Bottom