Msingi imara ni amani na ustawi (si amani peke yake)

Given

Member
Oct 11, 2010
82
39
Ndugu

Tukumbushane juu ya hili. Msingi wa kweli imara kwa nchi na watu wake ni umoja, Amani na Ustawi.

Tuekuwa tukikosea sana kwa kuhubiri amani na umoja peke yake! Tuijali nchi na watu wake wa sasa, na vizazi vijavyo. Tuongelee ustawi wa nchi na watu wake. Hapo ndipo vyote (amani na ustawi kwa pamoja) vitakuwa endelevu.

Viongozi (wa dini, siasa, serikali, n.k. ) hebu wajali kwa dhati nchi na watu wake! Msihubiri juu ya amani tu bila kujali hali halisi ya watu wake sasa, na baadae! Ni wajibu msimamie ustawi wao. Ustawi hutokana na maendeleo (kiuchumi, kielimu, kitechnolojia, kiafya, huduma zote za jamii n.k). Faida ya maendeleo ni ustawi wa jamii.

Hebu kila mmoja na awe na kujali! Tukatae maneno ya 'kisiasa' tu yakaziayo amani peke yake. Ni aibu, ni fedheha!

Kutokana na uduni wa hali ya jamii (kielimu, kiafya, kiuchumi), sasa wabaya wanapenyeza kirahisi sumu za hatari ktk jamii kama udini, ukabila n.k ili kulinda maslahi yao. Kutokana na umaskini na ujinga wa wengi, hoja za hatari kama hizo za udini zinaaaminiwa na kukubalika ktk jamii. Hii ni hatari kubwa kwa mustakabari wa nchi.

Tuwe wakweli, tujali nchi na watu wake. Tutafute, tusimamie na kuhimiza umoja, amani NA USTAWI! Huo ndio uzalendo wa kweli. Ni aibu, ni fedheha, ni dharau, ni kashfa kuongelea amani peke yake! Tuache!

Kila mmoja amuelimishe na kumhamasisha wa karibu yake juu ya hili, tuiponye nchi yetu na vizazi vyake!

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom