UKIONA UMEJIANDAA SANA NA VALENTINE UHUSIANO WAKO UNA UFA:
Taratibu tutaelewana tu..Unasubiria Ijumaa ya Tarehe 14 kwa nguvu sana ILI IWEJE???Labda kama ni Anniversary ya penzi lenu(mlikutana siku ya tarehe hiyo),kwamba ni muhimu kuadhimisha..Wewe penzi lako na mchuchu mmeanza June 12,Valentine inawahusu nini??Mwaka mzima ulikuwa wapi??
Watu wenye Mapenzi STRONG siku hii ni Ijumaa ya kawaida kabisa na wataenda SKYLIGHT tu Thai Village kama hamna kinachoendelea,ila WEWE na uhusiano wako wa Bagia na Chumvi ndo unataka Ufufukie Ijumaa..Halafu Jumapili Mzike tena mpaka mwakani.
Kwangu mimi Valentine ni kila siku...Nikikuta nguo nzuri ya bebe nanunua nampelekea,hata kama ni November 19...Nikimmiss namfuata ghetto tunaenda Dinner Capetown Fish Market kula...Akiona kiatu kizuri ananunua anani-surprise,hata kama ni August 7
Penzi lililokufa halitabustiwa na Valentine Day kamwe...Kama hupendwi hupendwi tu,Penzi halifufuki Ijumaa...Penzi lililojengwa kwenye misingi Imara huenjoy Valentine kila siku
Narudia tena,Ukiona umepania sana Ijumaa ujue Penzi lako lina shida kwa sababu hata LEO inaweza kuwa Valentine yako ukiamua.Penzi la kweli halina tarehe kama Kalenda.