Mcharo son
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 4,646
- 3,742
Habari nyote.
Msimamizi wa mirathi moja iliopitishwa mahakamani tayari hapa Tanzania, kamgawia mwanae nyumba ambayo ni mali ya marehemu.
Msimamizi huyu ni mdogo wa kuzaliwa tumbo moja na marehemu. Marehemu kaacha nyumba kadhaa na mashamba. Marehemu ameacha watoto wa kike na wa kiume. Watoto wote wamepata mgawo katika mali za marehemu japo wapo waliokuwa wanaona wamepunjwa.
Mtoto wa msimamizi wa mirathi (aliepewa nyumba) alikuwa anaishi pamoja na familia ya marehemu kama mwanafamilia kwa minajili ya undugu hakukuwa na mkataba wowote. Kwa kuwa alikuwa anaishi hapo mpaka marehemu alipofariki, basi baba yake ambaye ndie msimamizi wa mirathi na ndie mzee wa familia aliebaki na ndie aliepitisha mgawo na kumpatia mwanae nyumba, akidai kuwa ANASTAHILI kwa sababu aliishi katika familia ya marehemu na alikuwa anatekeleza shughuli za pale nyumbani kama mwanafamilia.
Marehemu hakuacha wosia wowote.Wapo wanandugu waliopinga kitendo hicho. Watoto wa marehemu waliafiki kumpa angalau kipande cha shamba lakini sio nyumba.
Msimamizi alifanikiwa kufanikisha njama zake kwa kupeleka mgawo huo mahakamani kwa kupitia shauri husika la mirathi kwa siri bila kuwaonyesha wadau na hakuwashirikisha wazee wenzake mpaka ilipopitishwa ndio akatangaza mgawo huo na kasema hakuna kupinga kwa kuwa Hakimu kapitisha saini tayari, HALI HII ILILETA MPASUKO NDANI ya wanandugu.(Wapo waliodai kuwepo na mazingira ya rushwa) Hakimu alicomment kuwa anapitisha shauri hilo kwa kuamini busara ya msimamizi wa mirathi husika.
Swali ni hatua gani stahiki inafaa kupinga ujanja huo. Maana aliyekabidhiwa nyumba amehesabiwa kama mototo wa marehemu kitu ambacho sio. Kikao cha ukoo hakikumholodhesha huyo mototo kama ana madai yoyote dhidi ya marehemu.