Msilete Mizaha na Babu wa Samunge bandugu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msilete Mizaha na Babu wa Samunge bandugu!!

Discussion in 'Jamii Photos' started by ngoshwe, Jun 7, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Cimg6472.jpg Cimg6418.jpg Cimg6476.jpg Cimg6474.jpg


  [​IMG][​IMG]


  Miongoni mwa matukio ambayo yanadaiwa kutokea kwa Babu Samunge ni pamoja na wezi kushindwa kuondoka na simua au fedha wanazo kwapua eneo hilo. Jana asubuhi nilikuwa Samunge, nilibahatika kuwahi sala ya asubuhi ya Babu ambapo katika mahubiri yake alihasa yafuatayo:
  (i) dawa anayotoa inatibu magonjwa yote sugu ikiwemo Ukimwi, Kifua kikuu, pumu, kisukari nk. alieleza dawa yake inaendana ana kuzingatia neno la mungu. Haina masharti, ila anadai wale wanaopata kikombe waendelee baada ya siku moja ya kunywa dawa kutumia vileo, nyama nk kwa kiasi. Ila kwa wenye HIV, waache kabisa "kutumiana salio" kwani kikombe ni mara moja tu (hakuna kurejea).
  (ii) aliwataka wananchi waliopo eneo hilo wasithibutu kukwapua chochote. Ikiwa wataokota chochote wakabidhi kwa wahudumu hapo.

  Awali nilisikia mengi yaliyowahi kutokea hapo ikwemo majaribio ya watu kutaka kupora nk.

  Kwa sasa usafiri shwari, kutoka Arusha Mjini mpaka kwa Babu na kurejea unaweza kwenda hadi kwa Tshs. 50, 000 tu magari ya kumwaga na zaidi ni matatu toka Nairobi na vitongoji vyake na pia Congo, Rwanda na Burundi . Wakati tukirejea, tulikuta gari moja likiwa limeungua barabarani (picha Na.1 hapo juu), ni karibu kabisa na mlima wa Oldoinyo Lengai.Dereva wetu akatujuza kuwa gari hilo liliungua mwezi Aprili na lilitokea Samunge kwa Babu lakini hakuna aliyejeruhiwa. Gari hilo lilikuwa huko na vijana wa kike na kiume (hawakujulikana walitokea wapi) ila inadaiwa walikuwa wakionyesha filamu zisizo na maadili ya Kitanzania wakiwa kwenye gari hilo kule Samunge. Japo hakukuwa na uthibitishio wa kutosha kuhusu chanzo cha ajali hii, lakini baadhi ya abiria iliwatia hofu kusikia haya!!!..wengine walisema "kweli Babu hafanyiwi mchezo".
   
Loading...