Msikilize mstahiki Meya wa jiji la Dar Yupo live Clouds Fm

RingaRinga

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,041
510
Anaongea katika kipindi cha jahazi,
Ntaendelea kuwapa updates

Updates;
Anasema wanaenda kuanza kazi maramoja kushughulikia kero za wana Dar es Salaam,
Usafi, Msongamano wa magari nk

Anasema wamelilia muda mrefu kupewa dhamana ya kuongoza, wameipata. Wataonyesha ndani ya miezi sita tofauti ya UKAWA na waliotangulia.

Updates;
Anahimiza watu walipe kodi na kodi zao zitafanya kazi za kuboresha maisha ya wana Dar kwa kiwango kinachokubalika.

Anasema kinamama ntilie watawawekea mazingira mazuri ya kazi kwa manufaa yao na watu wanaowahudumia ikibidi wawe na maeneo rasmi ili wateja wao wasikose huduma yao.

Updates;
Anasema bodaboda wanastahili kuruhusiwa kuhudumia hadi katikati ya jiji nyakati za asubuhi ili kuwahisha watu makazini, wataangalia uwezekano wakulifanikisha hilo
Kuhusu bomoabomoa anasema waathirika walipaswa waandaliwe viwanja vya kujenga badala ya vile walivyofanyiwa maana sio wengi 'kivile'

#Kibonde ndo alikuwa mwenyeji wake, wamemaliza.
Yaliyonipita ongezea
 
Anasema kinamama ntilie watawawekea mazingira mazingira mazingira mazuri ya kazi kwa manufaa yao na watu wanaowahudumia ikibidi wawe na maeneo rasmi ili wateja wao wasikose husuma yao.
 
Anasema bodaboda wanastahili kuruhusiwa kuhudumia hadi katikati ya jiji nyakati za asubuhi ili kuwahisha watu makazini, wataangalia uwezekano wakulifanikisha hilo
 
Kuhusu bomoabomoa anasema waathirika walipaswa waandaliwe viwanja vya kujenga badala ya vile walivyofanyiwa maana sio wengi 'kivile'
 
Huyu jamaa ana vitu tofauti sana na yule makonda ambaye kazi yake ni kuweka ndani anti
Ccm.Mungu akutangulie mayor wetu.kweli you were destined to be a great man
 
Yaani kama hoja ni mama ntilie na boda boda nakuwa na wasi wasi.

miezi sita kuibadilisha dar? ? ?
Anaongea katika kipindi cha jahazi,
Ntaendelea kuwapa updates

Updates;
Anasema wanaenda kuanza kazi maramoja kushughulikia kero za wana Dar es Salaam,
Usafi, Msongamano wa magari nk

Anasema wamelilia muda mrefu kupewa dhamana ya kuongoza, wameipata. Wataonyesha ndani ya miezi sita tofauti ya UKAWA na waliotangulia.

Updates;
Anahimiza watu walipe kodi na kodi zao zitafanya kazi za kuboresha maisha ya wana Dar kwa kiwango kinachokubalika.

Anasema kinamama ntilie watawawekea mazingira mazingira mazingira mazuri ya kazi kwa manufaa yao na watu wanaowahudumia ikibidi wawe na maeneo rasmi ili wateja wao wasikose husuma yao.

Updates;
Anasema bodaboda wanastahili kuruhusiwa kuhudumia hadi katikati ya jiji nyakati za asubuhi ili kuwahisha watu makazini, wataangalia uwezekano wakulifanikisha hilo
 
Si
Yaani kama hoja ni mama ntilie na boda boda nakuwa na wasi wasi.

miezi sita kuibadilisha dar? ? ?
Starajii alimaanisha atatumia kodi kuboresha maisha ya mamantilie na bodaboda, try to be fair while judging
 
Anasema bodaboda wanastahili kuruhusiwa kuhudumia hadi katikati ya jiji nyakati za asubuhi ili kuwahisha watu makazini, wataangalia uwezekano wakulifanikisha hilo
Huyu anaonyesha ni katika wale wanaopenda kufanya kazi ili wapate sifa, lini bodaboda kikawa chombo cha kusafirishia abiria, haoni hospitali zilivyojaa wagonjwa waliopata ajali za pikipiki na fujo wanazofanya pamoja na ujambazi, ilikuwa aseme atafanya bidii mabasi ya kasi yaanze kufanya kazi ili wananchi wapate usafiri wa uhakika.
 
Yaani kama hoja ni mama ntilie na boda boda nakuwa na wasi wasi.

miezi sita kuibadilisha dar? ? ?
Wasi wasi wa nn wakati kila kitu wazi.kasema boda boda asubui wafikiriwe maana kuna kuwahi hajasema boda boda wajiechie mjini siku nzima.sio kila kitu unaponda bana
 
unajua mtu wa kuibadilisha dar si yule wa kuja kuanza kusikiliza wale ambao alitakiwa kuwaongoza kwa maana ya ukiwa kiongozi unatakiwa uone kesho wakati unaowaongoza wao wanaangalia leo.

kubadilisha miji yetu hii inalazimu mtu aje na mipango ambayo mwanzoni itapingana na taratibu za maisha ya watu kwa sasa kwa maana watu wamekwisha zoea mfumo uliopo na kubadilisha staili wengi watalalamika lakini miaka mitano ni mingi hivyo mtu akijitahidi kuanza kufanya mabadiliko sasa huko mbeleni watu wataona kuwa mfumo aliouleta umeboresha maisha ya watu.

kwa kutathmini hii staili ya boda boda na mama ntilie ni mfumo wa kuangalia makundi ya watu walio wengi ukajiweka kwao ili ama kama fadhila au kama njia ya kuwashawishi kesho wakupigie kura.

kwa mfumo huu utafanya kile wanachokitaka na sio kuangalia mji kuweka utaratibu na kanuni za kila kitu ili kuboresha maisha au kuweka mambo sawa katika mji.

Wasi wasi wa nn wakati kila kitu wazi.kasema boda boda asubui wafikiriwe maana kuna kuwahi hajasema boda boda wajiechie mjini siku nzima.sio kila kitu unaponda bana
 
Meya akiamini kuwa uboreshaji wa jiji la Dar ni kutenda kile ambacho makundi fulani yanataka kwaajili ya kuwafurahisha, atashindwa, na wapinzani wetu watatudharau sana.

Meya aachane kabisa na fikra za pikipiki kuwa usafiri wa jiji, huo utumike nje kabisa ya jiji ili kupunguza ajali na kuondoa usumbufu kwa madereva wa magari. Mzazi mwenye hekima haogopi kumnyang'anya mtoto kisu kwa hofu ya kuwa atalia.

Dar inahitaji mipango mipya, mbinu mpya na fikra mpya. Barabara za mabasi yaendayo kasi ziongezwe. Malori yatengewe muda wa kuingia katikati ya jiji. Na baadaye utazamwe uwezekano wa kuingia kwa magari madogo kati kati ya jiji kwa kulipia. Hilo lifanyike baada ya kuboresha usafiri wa umma. Wenzetu kwenye miji kama Zurich, kuingia katikati ya jiji unalipia dola 50, wakieleza kuwa Zurich ni jiji la watu na siyo magari. Kule Perth, Australia maeneo yenye msongamano kama Karioakoo marufuku kuonekana magari zaidi ya vigari vidogo kwaajili ya walemavu vinavyotumia umeme. Magari mengine yote yanaruhusiwa kuanzia saa 5 mpaka saa 10 usiku.

Huu siyo muda wa kujipendekeza kwa watu. Ni muda wa kuchapa kazi. Kama kuna mambo mazuri aliyoyazungumza Makonda, meya ayachukue. Tunaichukia CCM kwa kuendekeza rushwa lakini kuna baadhi ya mipango ni mizuri, wameshindwa tu kuisimamia, sisi tuichukue na tuisimamie.

Kujitenga na Rais Magufuli haitamsaidia Meya. Aandae mipango yake, aende nayo kwa Magufuli, wabadilishane mawazo. Kama anayaoyafikiria kuyafanya yakaungwa mkono na Rais, utekelezaji wake utakuwa rahisi zaidi. Mimi ni CHADEMA hasa lakini naamini kuwa ili Dar iweze kubadilika tunahitaji sana ushirikiano toka kwa Mh. Rais, Mkuu wa Mkoa, madiwani wote, wenyeviti wa serikali za mitaa wote na wananchi wote. Tusiwatenge watu wenye mamlaka wa CCM au watendaji wa Rais kwa vile tu ni wana CCM. Tukifanya hivyo hatutakuwa tofauti na CCM inayodhani kama si miongoni mwao basi wewe ni adui.
 
Back
Top Bottom