Msijidanganye, CCM wana nguvu tu kwa sababu ya Rais Magufuli!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Msifanye kosa la kujidanganya kwamba mnaweza kumyumbisha Raisi wa JMTZ, usomeni upya mfumo wa TanZania Raisi ndiyo kila kitu na CCM na watu wake wanaonekana wana nguvu tu kwa sababu wana Dola yaani Raisi wa nchi ndiyo Mwana CCM lkn kinyume chake CCM siyo kitu, bila Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri CCM siyo kitu nchi hii, Mwenyekiti wa CCM atafanya nini bila ya Raisi wa nchi? Anabakiwa na nini? Anaweza hata akamuamrisha nani na akamsikia?

Ndiyo maana nasema kama ni vita ya CCM dhidi ya Raisi wa nchi basi huu ndiyo mwisho wa CCM kama tuijuavyo kwa maana hakuna CCM bila Dola, na hakuna Dola bila ya Raisi wa JMTZ!

Ndiyo maana hizi za akina Membe ni sarakasi tu za kutafuta attention lkn bifu hasa dhidi ya Raisi wa JMTZ CCM kama Chama hawawezi kuthubutubu kufanya, kwa maana Raisi ndiyo kila kitu TanZania!
 
Kakojoe kalale ukiamka nenda ufipa kachukue buku mbili yako.....shenziiiii
 
Je kuna ushahidi wowote ule kuwa CCM ambayo Magufuli ni mwanachama wake haina wengine kama yeye?. Mtu huja na kuondoka utendaji wa taasisi hubakia muda wote. Nadhani ni jambo la muhimu sana ikiwa vyama vyote vya siasa vitawekeza katika kujenga mazingira ambayo vipaji vya wanasiasa mahiri vitaweza kuonekana na kulisaidia taifa letu. Huu pia unaweza ukageuka kuwa muongo wa mwisho kwa vyama vya siasa kuachana na dhana potofu kwamba anaanza mtu na vipaji vyake halafu kinakuja chama cha siasa. Ukweli ni kwamba kinaanza chama cha siasa chenye taratibu, tamaduni na kanuni za uongozi halafu ndipo wanapoibuka wanasiasa. Kuamini katika watu kunaambatana na hasara za kufikiria katika kuwamaliza kisiasa hao watu na katika mchakato huo batili watapotezwa kisiasa watu wengi ambao Mungu kawajalia neema kubwa za uongozi.
 
Back
Top Bottom