Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 201
- 1,534
Kamishna wa Tume ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Peter Msigwa amesema uteuzi wa Katibu wa Bunge uliofanywa na Rais Magufuli hapo jana ni batili kwa kuwa ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi (null and void ab initio).
Hii ni kwa sababu uteuzi huo haukufuata taratibu zilizoelekezwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 87, ikisomwa pamoja na sheria ya utawala ya bunge ya mwaka 2016, kifungu cha 7(3), ambavyo vinaelezwa kuwa Katibu wa bunge atateuliwa na Rais kutoka kwenye majina matatu yaliyopendekezwa na kamati ya bunge.
Msigwa ambaye ni mjumbe wa Tume inayopaswa kupendekeza majina matatu kwa Rais, amesema Tume yake haijawahi kukaa, kujadili wala kupitisha majina ya watu wanaopendekezwa kuwa Katibu wa bunge.
"Mimi kama Kamishina wa Tume ya bunge hatujawahi kupendekeza majina ili Rais ateue katibu wa bunge. Serikali inaingilia bunge." ameeleza Msigwa.
Sheria inayomruhusu Rais kuteua jina moja kati ya matatu yatakayowasilishwa kwake na Tume ya bunge imetumia neno "shall" na siyo "may" kwa maana kwamba imemtaka Rais kutokwenda kinyume na matakwa hayo. Ni lazima afuate utaratibu huo. Lakini inadaiwa hakuna mapendekezo ya Tume yaliyokwenda kwa Rais. Yani amejiteulia tu bila kufuata Sheria wala Katiba. Zitto alihoji hilo pia jana.
Bado haijafahamika kama Rais hakujua utaratibu au alishauriwa vibaya na wasaidizi wake.