Ila wapinzani nao kwa kweli wanastahili kukimbiwa mana kwa hakika hawana mizizi.
Ni vyama vinavyoendeshwa kama BIKO .
Leo ipo kesho wameiondoa kwenye mtandao.
Hivi Mbowe haoni tatizo litakalotokana na kukosekana kwa ofisi za chama kuanzia Taifa mpaka kwenye mashina au mitaa?
Kukosa ofisi ni sawa na kijana aliyeoa na kuishi maisha yake yote bila kuwa na sehemu ya kuishi au kujenga nyumba.
Siku akikorofishana na mke wake familia inasambaratika mana watoto wengine wataenda kuishi kwa bibi mzaa baba wengine bibi mzaa mama na wengine kwa wajomba n.k.
Ofisi zinazojengwa na chama ni mali hivyo zinawafanya wanachama kuwa wavumilivu na kulinda mali zao.
Chama kikiwa na mali zake hakuna mtu anayewaza kukiacha chama na nguvu zake zikapotea bure.
Hii tabia ya Mbowe kuendelea kukikopesha chama mpka vitu vidogo vidogo ambavyo wanachama wangehamasishwa wangechangia ni hulka mbaya kabisa ya kukiona chama kama mali yake binafsi na hapo ndipo patakapoleta taswira ya VICOBA badala ya chama kinachotazamiwa kushika dola.
Hiyo mipango mingi wanayojifanya hao wapinzani kuiandaa na kuikosoa serikali kwenye bajeti ya kila mwaka kwa nini hatuioni wakiipanga kwenye chama chao tukaona kinaibuka ghafla na kuipiku CCM kimiradi na kimapata yanayotokana na ubunifu wa miradi mingi yenye kujenga chama na kutoa hata ajira kwa vijana ili wasiwe na mawazo ya kukimbia kimbia?
Tatizo ni moja hawaaminiani!
Ndio maana kila mtu anayeingia upinzani hasa Chadema anatoka haraka mana anaona kama ametemgwa na hakuna mikakati zaidi ya matamko!
Jipangene ,tafuteni watu makini wenye maono mapana msijione kuwa mko sawa. Kubalini mawazo mapya na pia kukosolewa.
Mnalaumu serikali ya awamu ya Tano kuwa haishauriki lakini nanyi pia mna tabia hiyo hiyo. Mkishauriwa mnatoa lugha chafu na za kejeli. Ni udikteta nao huo.
Nakumbuka Mh. Rais alimshauri Mbowe kuwa chadema kijenge Ofisi yake Dodoma kwa kuwa makao makuu yatahamia huko mapema.
Mpaka leo hawana ofisi huko wakati ile ilikua ni fursa kubwa ya kujitangaza kisiasa.
Siasa ni maendeleo sio porojo majukwani tu. Kila jambo linalogusa jamii likitumika vizuri ni siasa na linaweza kujenga chama.
Hivi Kweli Mtu alikua Waziri anahamia chama ambacho hakina hata Ofisi.
Ofisi ya kanda inakua kama Frem ya duka la Mangi halafu kweli mtu huyo akiitwa tena CCM kwa ahadi ya kupata maslahi na mazingira mazuri ya kisiasa asiruti? Thubuutu sio kwa nchi hii ambayao CCM ina makada mpaka kule kwenye walinzi wakubwa kabisa wa madola.