Msichana hatarini kuuzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msichana hatarini kuuzwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Acha Uvivu, Jan 24, 2012.

 1. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wana Jf nimetumia kichwa hicho hapo juu kufuatia masikitiko na maumivu anayoyapata msichana aliyepoteza wazazi wake na kuchukuliwa kukaa na shangazi yake anayemlazimisha kuolewa na mwanaume asiyemjua.

  Mwanzoni mwaka jana msichana mwenye umri wa miaka 17 akiwa Form 2 katika wilaya Ifakara akafiwa na mama yake.
  Baada ya maombolezo, ndungu wa karibu wakakaa namna wanavyoweza kuwasaidia watoto wa marehemu, ambao pia walishapoteza baba yao mzazi. Shangazi yao mmoja (hapa Dar) anayefanya kazi ya mama ntilie akaomba kuondoka na huyu msichana, kwa ahadi kwamba atamsaidia kumhamisha shule ili aweze kuhitimu. Ndugu wote wakakubali (mwezi wa nne, 2011) kuwa amchukue. Alipofika kwake huyu mdada akawa anamsaidia huyu shangazi yake kuandaa chakula pamoja na kuwahudumia wateja.

  Mwezi wa kumi, 2011 muda wa kufanya unyago ukafika na wakarudi huko Morogoro kukamilisha hiyo shughuli. Kadiri muda ulivyoenda, huyu shangazi hakuwahi kumweleza huyu dada kuhusu mpango wa kupelekwa shule. Baadaye akaitwa na kuambiwa kuna mzee alifika nyumbani kwake huyu shangazi na akawa amevutiwa na huyu dada. Hivyo akaomba kijana wake huyo mzee amuoe huyu binti. Shangazi akakubali na kumueleza huyo binti, anayesema hakumjibu kitu baada ya kuambiwa ila alipokea kwa mshituko hiyo kauli ya shangazi yake.

  Bila kumkumbusha shangazi juu ya ahadi yake, huyu binti akaenda kwa mjomba (mume wa huyu shangazi) juu ya nia yake kuendelea na masomo. Mjomba akamuahidi kumsaidia. Hivi juzi tu kijana wa yule mzee akafika na gari akiongozana na kaka wa huyu binti ktk ukoo-wote toka Gongo la Mboto.

  Kwanza huyu jamaa akaonana na huyu shangazi pamoja na mjomba (mume) wakazungumza na baadaye kumwita binti. Binti akafika na kuelezwa kuwa mume mtarajiwa ndo alishafika. Binti akakaa kimya. Jamaa akauliza mbona nimeambiwa na mzee wangu kuwa mlishazungumza? Mbona binti haonyeshi mwelekeo? Mjomba (mume) akajibu sijui wenyewe sitaki kuwa shahidi, akaondoka.

  Baadaye wakashauriana kwamba wabaki wawili wazungumze. Mdahalo ulikuwa hivi:

  Njemba; Mimi nilikuwa na mpenzi wangu, tulipendana sana, lakini wazazi wangu hawakumpenda sababu Mzalamo. Tumeachana hivi juzi tu na anazidi kuumia. Hivo nimekupenda nataka nikuoe.

  Binti: Umenipenda saa ngapi, leo si ndo mara ya kwanza kuniona?

  Njemba; Ndio na tayari nimelizika na wewe.

  Binti; Sijui nyie wenyewe maana mimi mipango yangu ni kwenda shule na sio kuolewa.

  Njemba; Usiwe na wasi wasi baba yangu atakupeleka shule.

  Mazungumzo yakaendelea baadaye mwanaume akashindwa na kuondoka. Baada ya wiki moja binti akamfuata tena mjomba (mume wa shangazi) kuhusu shule. Akamjibu tayari ameshaongea na mkuu wa shule ya Sekondari (hapa hapa Dar) suala ni vibali toka shule ya huko Moro na sijui kama yupo anayeweza kushughulikia. Binti akajibu yupo.

  Binti akajaribu kuwasiliana na mamake mkubwa aliyeko huko. Bahati mbaya akajibiwa kuwa anauguza mume wake hivo hatoweza.

  Binti ana mpango wa kwenda Moro akafuatilie mwenyewe. Lakini kuanzia jana shangazi yake hamtazami vizuri. Kisha huyo shangazi akaropoka "eti anataka shule, sijui ya kusomea umalaya". Binti akaishiwa nguvu.

  Ndugu wana jf, huyu dada ni miungoni mwa watoto wengi ambao wanataabika ktk jamii yetu. Tumsaidie japo kwa ushauri maana anaumia sana na anaonekana anapenda asome. Nipo tayari kujibu pale ambapo panaonekana kutoeleweka. Nawasilisha.
   
 2. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ongeza font pia weka paragraph, macho yanauma kusoma ikiwa hivo.
   
 3. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sawa mkuu, ila niwie radhi natumia Nokia Classic hivyo siwezi kuweka paragraph na kuongeza font. Naomba wanajf wengine angalau kujitahidi tu kuisoma na angalau kutoa ushauri.
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mkuu story yako ni mzuri na inasikitisha sana ukizingatia binti anataka kusoma! Niwie radhi ili story yenyewe iweze kusomeka na isiwape shida wana JF nimeifanyia Edit kidogo natumaini hutajali.
   
 5. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa kufanya hivyo mkuu.
   
 6. M

  Maga JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 325
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  je wewe huyo binti ni nani yako?
   
 7. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hatuna undugu wowote. Kwa sababu tu ya kufahamiana ninapoenda kupata chakula, ndipo akaniomba namba ya simu na kunielezea hayo baadaye.
   
 8. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wana jf nimeweza kurekebisha (editing). Sasa inaonekana na kusomeka vizuri.
   
 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ngoja nisome kwanza, maana ilikuwa haivutii kuisoma
   
 10. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huyo binti ni under age, mwambia aka report police kitengo cha wnawake na watoto, pale makao makuu (mambo Ya ndani) watamsaidia
   
 11. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sawa, ingawa pia nilijaribu kumshauri hivyo lakini anaonekana ni mwenye huruma sana inapofika hatua inayoweza kuwakwaza hao ndugu zake. Na pia ieleweke kuwa kwa sasa anaweza akawa amefikisha miaka 18 tayari.
   
 12. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  mtoa hoja toa mapendekezo sasa maana wewe angalau unajua hali halisi, kwa maana ukiwa mwelewa unaweza kujua kama kweli binti anataka kusoma au la!
   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Aende ofisi za ustawi wa jamii kwenye wilaya aliyepo,pia kuna kitengo kinachoshughulikia masuala ya kifamilia katika vituo vingi vya polisi na wengi wa wanaoshugulikia kesi kama hizi ni polisi wanawake,aende kwanza huko,nina hakika atapata mwanzo mzuri katika kutatua tatizo lake.
   
 14. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa ushauri wako. Bila shaka ushauri mnaotoa wanajf nitaufikisha.
   
 15. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Msaidie haraka sana kwa kuwasiliana na TGNP na ile taasisi ya mke wa JK inaitwa WAMA. Wanayo WAMA NAKAYAMA SEC SCOOL, nadhani watamsaidia, Contacts za wama ni box 10641 dsm, simu +255222126516 Fax +255 222121916, email info@wamafoundation.or.tz Tayari nimewaforwadia hii page, sijui kama wana tabia ya kusoma connent za email yao.
   
 16. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukuru sana, hapa naamini umeenda mbali zaidi ya ushauri. Nitamuelewesha juu ya hizo contacts na pia kumsaidia na taratibu za msingi kuwafikia hao TGNP, WAMA n.k
   
Loading...