kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Mwili wa msichana aliyefariki dunia baada ya kubakwa kweye basi nchini India umechomwa katika maziko yaliyohusisha watu wachache.
Mwili wa binti huyo uliwasili mjini New Delhi juzi siku moja baada ya kufariki katika hospitali moja nchini Singapore alipokuwa akipatiwa matibabu katika majeraha aliyopata baada ya kubakwa na kupigwa.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo, serikali iliwafungulia mashtaka wanaume sita kutokana na kuhusishwa na mashtaka hayo ya kubaka. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msomaji mashtaka alisema kuwa watu hao watakabiliwa na adhabu ya kifo ikiwa watapatikana na hatia.
Kitendo hicho cha ukatili kilichofanywa kwa mwanamke huyo kilizusha ghasi nchini India baada ya kufanyika kwa maadamano makubwa kuhusu vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake. Zaidi ya watu 2000 walifanya maandamano ya amani mjini New Delhi, kwa ajili ya kuitaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwalinda wanawake.
Kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi nchini humo, kila baada ya saa 18 tukio la ubakaji huripotiwa mjini New Delhi.
MWANAMKE HUYO ALIBAKWA NA KUNDI LA WATU NA KUSABABISHA VIUNGO VYA MWILI WAKE KUSHINDWA KUFANYAKAZI.
Source by: Mwananchi.