Mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris auawa

Mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris auawa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,852
Reaction score
63,370
Mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud, ni miongoni mwa watu waliouawa katika msako mkubwa wa polisi uliofanyika kwenye kitongoji kimoja kaskazini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris, Abdelhamid Abaaoud

Mwendesha mashtaka mkuu wa Ufaransa, Francois Molins amethibitisha leo kuwa mwili wa Abaaoud ulikutwa ukiwa na majeraha mengi, baada ya msako huo uliosababisha kiasi ya watu wawili kuuawa, akiwemo mwanamke mmoja anayedhaniwa kujilipua kwa kujitoa mhanga.

Molins amesema Abaaoud mwanamgambo wa kundi lenye itikadi kali la Dola la Kiislamu-IS, raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 28, anatuhumiwa kupanga mashambulizi ya Paris usiku wa Ijumaa iliyopita yaliyowaua watu 129 na kuwajeruhi wengine 352.

Awali polisi walidhani Abaaoud yuko Syria, lakini upelelezi wao uliwaongoza kwenye nyumba moja mjini Paris katika kitongoji cha Saint-Denis na maafisa wa jeshi waliokuwa na silaha nzito waliivamia nyumba hiyo kabla ya kuiharibu kabisa.
Uchunguzi wa kutambua alama za vidole umetumika kuutambua mwili wa mtuhumiwa huyo mkuu, ambaye mwili wake umepatikana kwenye kifusi cha jengo lililovamiwa na vikosi vya usalama na kushambuliwa kwa risasi na mabomu.

Waziri Mkuu apongeza

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls amepongeza hatua ya vikosi vya usalama vya Ufaransa kwa kufanikisha mauaji ya Abaaoud, baada ya kufanya msako mkubwa mjini Paris.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls

''Wengi wenu tayari mnajua, lakini nashukuru operesheni iliyofanyika jana. Mwendesha mashtaka mkuu wa Ufaransa amethibitsha kwamba sasa tunajua Abaaoud, aliyepanga mashambulizi, ni miongoni mwa waliouawa katika msako wa vikosi vya usalama,'' alisema Valls.

Valls ameonya kuna hatari huenda IS wakatumia silaha za sumu au vijidudu dhidi ya Ufaransa, na kusema kuna haja ya kuchukua tahadhari iwapo chochote kitatokea.

Aidha wabunge wa Ufaransa wameidhinisha kurefushwa kwa muda wa hali ya hatari nchini humo kwa kipindi cha miezi mitatu, pamoja na kuidhinisha kufungwa mitandao kama kuna haja ya serikali kufanya hivyo katika kipindi hicho.

Maafisa wa kijeshi wa Urusi na Ufaransa wakutana
Wakati huo huo, mkuu wa majeshi wa Urusi, Jenerali Valery Gerasimov na mwenzake wa Ufaransa Jenerali Pierre de Villiers wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu hii leo, ambapo wamejadiliana kuhusu ushirikiano wa kijeshi na hatua za kuchukua dhidi ya magaidi wa IS nchini Syria.

Kansela Angela Merkel

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uhispania, Jorge Fernandez Diaz amesema Abaaoud alijaribu kuwapatia mafunzo ya kigaidi wanawake wanaoishi Uhispani kupitia mitandao ya kijamii, ili waweze kujiunga na IS.

Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameitaka jumuiya ya kimataifa kusimama pamoja katika mapambano dhidi ya ugaidi. Wito huo ameutoa leo mjini Berlin wakati akizungumza na kiongozi mwenzake wa Austria, Werner Faymann.

Yote hayo yanajiri wakati wakati ambapo jeshi la muungano wa kimataifa linaloongozwa na Marekani likiwa limefanya mashambulizi 19 ya anga dhidi ya IS nchini Iraq hapo jana, karibu na Kirkuk, Kisik, Mosul, Ramadi na Sinjar. Marekani imesema jeshi hilo pia limefanya mashambulizi manane ya anga dhidi ya IS nchini Syria.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo/RTRE,AFPE,DPAE,APE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 
151118192915_abdelhamid_abaaoud_512x288_ap_nocredit.jpg
Image copyrightAP
Image captionAbaaoud anadaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129Mwendesha mashtaka nchini Ufaransa amethibitisha kwamba mwanamume aliyetuhumiwa kupanga mashambulio ya Paris aliuawa kwenye operesheni ya jana.
Abdelhamid Abaaoud ndiye aliyekuwa akisakwa na polisi waliovamia nyumba moja katika mtaa wa Saint Denis, kaskazini mwa Paris jana.Awali, mwendesha mashtaka wa Paris Francois Molins alikuwa amesema Abaaoud na mshukiwa mwengine Salah Abdeslam hawakuwa miongoni mwa watu wanane waliokamatwa.Hata hivyo, miili ya watu wawili waliouawa ilikuwa bado haijatambuliwa na baada ya uchunguzi imebainika kwamba Abooud aliuawa.Hayo yakijiri, wabunge nchini Ufaransa wanatarajiwa kupiga kura kuongeza muda wa kutekelezwa kwa hali ya hatari.Wapiganaji wa Islamic State (IS), ambao wanadhibiti maeneo ya Syria na Iraq walisema ndio waliohusika katika mashambulio hayo yaliyoua watu 129 na wengine 400 kujeruhiwa Ijumaa.
Gazeti la The Washington Post awali lilikuwa limenukuu maafisa wa Ulaya ambao hawakutajwa majina yao wakisema Abaaoud, 27, aliuawa kwenye operesheni hiyo ya polisi Saint Denis.

Source BBC

 
Wahuni wachache wanachafua hali yahewa, Kova anakomaa anasema eti Magaidi. Ugaidi ni mbaya sana Kova akajifunze Kenya tu.
 
Pamoja na kutokufurahia mambo haya ya hivi vikundi lawama kubwa sana ziwaende mataifa makubwa ambao ndiyo huwapa silaha na mafunzo ya kwenda kupigana kuondoa viongozi ambao wakubwa hao huona kuwa wamekaa muda mrefu madarakani,matokeo yake hivi vikundi huja kuwa ni tatizo kwa hao wahisani wao. Nani asiyejuwa kuwa ISIS walikuwa wanapewa misaada na Amerika?
 
ni mshukiwa tu...kwanini watumie nguvu hvyo kumkamata bila hata ya kumuhoji...nguvu kubwa inatumika
 
Back
Top Bottom