Mshindani wa kiuchumi wa Tanzania EA ni nani?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,316
38,455
Katika ukanda wa Afrika Mashariki mshindani wetu kiuchumi ni nani, na tunashindana naye zaidi kwenye sekta ipi? Sisi kama taifa tunamiliki asilimia ngapi ya soko la Afrika Mashariki na wenzetu wanamiliki kiasi gani cha asilimia kwenye soko letu la ndani?
 
Kenya ilitupita mwanzoni mwa 2000s sahizi Iko miles away ila kwa kasi ya JPM tutakula nao sahani moja soon
 
Heri ya Mwaka Mpya @Allen Kilewella

Mshindani wetu kiuchumi ni Kenya, especially kwenye tourism and transportation sectors. Kwa bahati mbaya au mzuri, Kenya wana rais ambae ni capitalist before being a president na unapokuwa na rais wa aina hiyo, wakati wote atahangaika kutumia mbinu mbalimbali ili kuiwezesha nchi yake kuhodhi soko coz' anakuwa ameua ndege wawili kwa jiwe moja... mafanikio yake mwenyewe na ya nchi yake.

Kutokana na ukweli huo, ndio maana moja ya mbinu ambazo Kenyatta alizitumia ni kummaliza mshindani wake Tanzania kwa kuanzisha umoja mwingine ndani ya umoja wa EA! Huo umoja mwingine ni ule ambao ulitambulika kama Coalition of Willing! Lengo la Kenyatta kwenye umoja ule ilikuwa ni kutaka kuhodhi transportation and tourism sector in the region.... Uganda na Rwanda wakaingia kichwakichwa! Tanzania ika-refrain lakini kwa kuwa Watanzania sisi ni watu tusiopenda kufuatilia mambo na matokeo yake kuishia kukurupuka; tukaanza kuilamu serikali na kumkejeli JK kwamba ni goi goi... kwamba wenzake wanakimbia, yeye analala usingizi!

Pamoja na makosa yote ya JK, hakuna jambo ambalo serikali yake ili-handle vizuri basi ni hili la East Africa. Hapa ninaposema ile inayoitwa Coalition of Willing inapumulia mashine baada ya Kagame na Museven kushituka kwamba Kenyatta anawapelekesha! Hapa ninaposema Museven ametupa jicho lake Sudan ya Kusini na Kagame amerudi Tanzania na mwezi May mwaka jana wakakubaliana kujenga reli ya pamoja itakayounganisha Tanzania, Rwanda na Burundi ambayo inafahamika kama Dar es Salaam‐Isaka‐Kigali/Kesa‐Musongati Railway ambayo itachukua muundo wa TAZARA!!

Kwa namna moja au nyingine, hofu imetawala mradi wa reli ya standard gauge kule Kenya baada ya Rwanda kuingia rasmi Tanzania. Tegemeo pekee la Kenya limebaki kwa Uganda ambae kwa sasa ni kama imechukua likizo ikielekeza nguvu zake South Sudan! Na ni hii South Sudan ndiyo hasa itakayoibua conflict of interest between Kenya and Uganda.

Huyu Kagame nilipata ku-doubt intelligence yake alipoingia kwenye mtego wa wajanja Kenya na kukubali haraka haraka kuingia kwenye Common Visa ambayo Tanzania tuliotolea nje!

Alamsiki... wacha niendelee na vacation yangu!!!
 
Kenya ilitupita mwanzoni mwa 2000s sahizi Iko miles away ila kwa kasi ya JPM tutakula nao sahani moja soon
Haahaha mzeee it will take10 plus years ku catch up with Kenya au ku surpass mana mhh
 
Back
Top Bottom