Wamekosa utu na huruma kabisa kwa wananchi na walipa kodi. Angalia mishahara yao ilivyo mikubwa na wanaipokea bila aibu kabisa il hali haikatwi kodo lakini bado wanamkandamiza mtumishi ambaye hafikii haata theluthi ya mishahara yao kwa kumkata kodi kubwa eti PAYE, wao PAYE wanakatwa wapi?
Bado wameongeza kodi kibao zisizo na kichwa wala miguu...unajua nini BAK wao machungu hawayasikii sbb kila kitu wanapewa tu hawana machungu yoyote ya kutafuta kwa jasho. Lakini ole nakwambia muda wao utafika watakapoinamisha vichwa vyao kwa aibu. Siku Mungu atakapoamua kusimama na kuanika uovu huu hadaharani.
Viongozi kama hao kamwe hawatataka mabadilko,kwasababu wengi wao kilichowapelekea ndo hicho(siyo kuelimisha,kuwatumikia wananchi na kuwafumbua macho),na wanajuwa wakiwafumbua macho wananchi,basi maslahi yao yatakuwa hayana maana na hawatafanya hivyo,bali kuendelea na shughuli ambazo wana maslahi nazo...Mfano kuhonga kanga na pilao,kuleta machafuko kwa kuhubiri chuki za kidini na kikabila,mauwaji,kweka fedha akaunti za nje,kuhakikisha wananchi hawajui haki zao na pia hawaeleimiki na kufahamu haki za uraia!
Mfano hata hapa JF,hawataki hoja zijadiliwe tena,kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kwenye hilo kwasababu kuna watu wanajibu upumbavu wao,wanaanzisha thread za kipumbavu na watu wana jibu,nadhani wanaofanya hivyo ni wale wanaotaka kujionyesha kwamba wanauwezo wa kupambana na maadui wa chadema na kutaka kuonyesha udhaifu wa mleta hoja,lakini the best weapon fo a fool is to ignore him.
Sisemi kwamba msijibu kila posti za hao watu,ila kama ni zakijinga kama aliyoitoa,msijibu!hata akianzisha thread ya kijinga,ignore it.!kuijibu ni faida kwake kwasababu hata mkimtukana,yeye anajuwa ni "the truth pain",licha ya kwamba si kweli.Kuwa mwanachadema makini,si kujibu hoja za fools!Ni kuunga mkono hoja zenye akili,kuelimisha,na kurespond kwenye hoja ambazo utaweza kuwaelimisha wananchi kwenye process ya kurespond,ama kusaidia kwenye udadavuaji pale inapotokea kuna mwenye honest question nk.