Binafsi nahisi kuna mkakati mkubwa na wa dhati unaotakiwa kuchukuliwa na serikali badala ya kukumbizana na inflation tena kwa kundi dogo tu la waajiliwa, wakati tunaambiwa zaidi ya Asilimia 80% ya Watanzania wako kwenye sekta isiyo rasmi. tunapozungumza sasa hivi lita moja ya mafuta ya taa ni zaidi ya sh 2000/= wakati si zaidi ya asilimia 15% ya Watanzania wa access na umeme wa mgao, maharage mboga ambayo inatumika na watanzania wengi kuliko yeyote leo hii kilo ni sh 2,000/= Namshauri Mh Rais asidanganywe atafakali na kuchukua hatua madhubuti juu ya maisha ya watanzania million 41 ambao amebeba dhamana yao.