Mshahara Makete kizungumkuti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshahara Makete kizungumkuti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by usungilo, Oct 6, 2012.

 1. u

  usungilo JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 501
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Watumishi wengi wa serikali hasa walimu jana walimiminika nmb ili kuweza kupata chao. Nyuso za watumishi hao zilibadilika baada ya kuona akaunti zao haziso hatua iliyopelekea wengine kurudi nyumbani kwa miguu badala ya kupanda usafiri kama walivyozoea hivi karibuni. Hii inasemekana imetokana na mfumo wa ulipaji ulioanzishwa ili kubana ulipaji wa watumishi hewa. Inaonekana kwenye mfumo huo mtandao wa ulipaji utakuwa unasoma mpaka makao makuu kwa kila mfanyakazi wa serikali. Kuna watu walipelekwa semina ya namna ya kulipa mishahara kupitia mfumo huo lakini hawajawahi kuutumia tangu warudi. Mwezi huu wamelazimishwa kuutumia kwani bila hivyo hawaruhusiwi kulipa watu mishahara. Kilichotokea ni kwamba transaction zilipofanyika ikaonekana kuna deficit kubwa ndani ya mfumo huo katika wilaya hii hivyo fedha nyingi zimekatwa kufidia deficit hiyo na kubakia salio kidogo linalosoma kwa mishahara. Sasa hivi wanahangaika namna ya kuyaweka mambo sawa ila haifahamiki mishahara itakamilika lini!
   
Loading...