Mseto wa Choroko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mseto wa Choroko

Discussion in 'JF Chef' started by MadameX, Sep 24, 2012.

 1. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mahitaji

  1/2 kg Mchele uliooshwa na kulowekwa.
  1/4 kg Choroko zilizooshwa
  1 cup Coconut powder
  11/2 tsp Chumvi

  Maelekezo

  Chemsha choroko mpaka ziive, halafu bandika sufuria yako ya maji ya mchele, acha ichemke. Mimina mchele wako acha kwa muda wa dakika 5-7 kiini kiive. Unamwaga maji, ya huo mchele unabakisha kiasi tu, tia choroko, chumvi na nazi yako ambayo umeikorogo na maji kidogo, geuza geuza ili vichanganyikane vizuri. Funika vizuri ili mvuke usitoke kabisa, punguza moto uwe mdogo sana. Acha iive kwa muda wa dakika 20-25, unaweza kugeuza tena ili ishikane vizuri.

  Tayari kwa kuliwa. Mimi kama mimi napenda ikiwa mseto wa nazi basi inaenda na supu. Ikiwa mseto wa bila nazi, ule uliopikwa na mafuta napendelea na mchuzi wa nazi, nyama au samaki.
   
 2. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe ni mtoto wa pwani! Basi kwa mchuzi wa nazi wenye pweza, mmmh!
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kitu cha kupika then unamwaga mchuzi unatia maji huwa sipendi sana kwa kuwa kinachobaki ni makapi na utamu tu vitamini hakuna.

  so huwa naweka maji kidogo sana ili kubalance nisimwage kitu ili kuongeza kitu vyote nitaweka bila kumwaga supu au mchuzi. chakula kama dawa na si chakula kama utamu.
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Rubi maji unapunguza ili huo mseto usiwe maji maji sana. Na hayo maji ni ya kukochanganyia hiyo coconut power.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hii imekaa poa sana hasa uishushie na juisi ya parachichi.. hatari wewe...
   
 6. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kwa hapo sawa my dear nimekupata. Kiukweli huwa sipendi kumwaga supu maana kuna watu utakuta anapika maharage au njegere au hata nyama mpaka zinakauka halafu akiwa anaunga anaongeza maji kwa ajili ya kupata mchuzi sasa huwa nawauliza kwa nini usipike moja kwa moja na ukabakiza supu kwa ajili ya kuungia mchuzi. huwa nakosa jibu.
   
 7. MSEZA MKULU

  MSEZA MKULU JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 3,733
  Likes Received: 4,586
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa vyema. Ngoja tuingie kwenye practical.
   
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Pweza tena!!! Mie napita tu vitu vingine tutaishia kuharisha bureee.
   
 9. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa ninyi wa madongo kuinama, lazima hali itakuwa hivyo. Waachieni wenyewe. Hahahaaaa!!
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  halafu unatupia kati kachori na chachandu pilipili
   
 11. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii kali! Hapo ndio yatakapokukuta ya @Young Master.
   
Loading...