Msemaji wa upinzani, David Silinde agoma kumuita Naibu Spika mheshimiwa na kuzua zogo

Mbunge wa Momba na msemaji wa kambi ya upinzani David Silinde ameingia bungeni kusoma bajeti ya upinzani lakini hakutaka kumuita naibu spika mheshimiwa na kusababisha zogo


Namuunga Mkono Shilinde Kwa asilimia 100% Jamii yetu ina matatizo makubwa sana. Hasa hawa wabunge na baadhi ya viongozi wanapenda sana kujikweza na kulazimisha kuitwa waheshimiwa.

Huwa najiuliza sana ni kitu gani ambacho wamekifanya kikubwa sana katika jamii mpaka wao wajione ni exceptional na waitwe waheshimiwa. Kwani ukiitwa ndugu fulani utapungukiwa kitu gani?

Jamii yetu watanzania tumelogwa siyo bure. Acha watu wakuite Mheshimiwa wenyewe kutoka na mchango wako katika jamii.

Hii inanikumbusha siku Wiliam Ngeleja wakati akiwa waziri alivyoenda kutoa pesa kwenye ATM machine, badala ya kutoa pesa anaongea na simu tu huku watu wengi wako kwenye foleni wanasubiri huduma.

Mlinzi kumwambia akaepembeni ili wateja wengine wapate huduma, eti akaanza kumtolea yule mlinzi vitisho. "Hujui mimi ni Mheshimiwa"? So, what?
 
Mbunge wa Momba na msemaji wa kambi ya upinzani David Silinde ameingia bungeni kusoma bajeti ya upinzani lakini hakutaka kumuita naibu spika mheshimiwa na kusababisha zogo

UKAWA mbona wana viherehere sana? Si walisusa? Sasa wanaingia kusoma budget ya nini ikiwa hawato changia? Hivi kwanini wasirudi tuu? Mbona hawatulii na kwanini hawana msimamo?
 
Namuunga Mkono Shilinde Kwa asilimia 100% Jamii yetu ina matatizo makubwa sana. Hasa hawa wabunge na baadhi ya viongozi wanapenda sana kujikweza na kulazimisha kuitwa waheshimiwa. Huwa najiuliza sana ni kitu gani ambacho wamekifanya kikubwa sana katika jamii mpaka wao wajione ni exceptional na waitwe waheshimiwa. Kwani ukiitwa ndugu fulani utapungukiwa kitu gani?
Jamii yetu watanzania tumelogwa siyo bure. Acha watu wakuite Mheshimiwa wenyewe kutoka na mchango wako katika jamii. Hii inanikumbusha siku Wiliam Ngeleja wakati akiwa waziri alivyoenda kutoa pesa kwenye ATM machine, badala ya kutoa pesa anaongea na simu tu huku watu wengi wako kwenye foleni wanasubiri huduma. Mlinzi kumwambia akaepembeni ili wateja wengine wapate huduma, eti akaanza kumtolea yule mlinzi vitisho. "Hujui mimi ni Mheshimiwa"? So, what?
Nakupongeza sana mkubwa kwa kutoa pongezi kwa David silinde maana ameamua kuwacha unafiki yaani umuite mtu mheshimiwa wakati wewe anakudharau?
 
video source:
katika hali ile ile ya kushangaza na kuendelea kwa sakata la naibu spika wa serikali (sio bunge) leo katika uwasilishwaji wa bajeti mbadala ya kambi rasmi ya upinzani iliokuwa ikiwasilishwa na mbunge wa momba Mh silinde, mh Silinde alifika kwenye podium ya kuzungumzia na kuanza kuzungumza pasipo kumtaja wala kuadress kwa naibu spika wa serikal Dk. Tulia Ackson hali iliopelekea wabunge wale wale wa chama kimoja kuanza kulia lia na kutaka afanye kumtambua naibu spika huyo wa chama na serikali, baadae nae mwenyewe alikazia swala hilo na kupelekea mvutano kidogo. kupitia hali hii kuna haja ya wabunge wa ccm kujitambua kuwa wao ni wabunge na sio serikali na wafanye kaza waliotumwa na wananchi.

source link video;

NOTE;- Mada hii inahitaji ubongo kufikiria na kujadili wale wakata viuno na wauza kahawa wa lumumba povu tuliache tuvae uzalendo na kujadili kitaifa

CHADEMA tangu iuziwe tajiri el kina vision moja tu. kuona el ndio anakua prezida.
 
Nchi hii ukitaka upate umaarufu wa ghafla, jibu ovyo,vunja kanuni, tukana matusi hadharani hasa kwenye serikali.....utaonekana shujaa hata kutunukiwa.!

Upinzani unapenda kudili na vitu vidogo vidogo ambavyo havimsaidii mtu wa kawaida zaidi ya kupata umaarufu wa muda kwenye mitandao ya kijamii.

Kuna haja ya upinzani kujitafakari upya na kuja na hoja za Msingi ambazo wenye akili watawaelewa.

Siasa za kishabiki na umaarufu wa siku moja hazitusaidii kama Taifa.
 
Back
Top Bottom