Msemaji wa Serikali: Kuna watu hawajamuelewa Rais Magufuli, Ni mtendaji na sio mwanasiasa

Mwambie tukutane 2020 kwenye kupiga pushup..najua atakuja na boxing ths tym

Jamaa atapeta tu 2020 tena kwa mbinde, kwa kweli hatujawahi kuwa na rais mchapakazi na mtendaji wa ukweli kama Magufuli, iliyobaki ni kumshukuru Mungu tu kwa kutupa yeye. Kwa kweli sioni haja ya kumpigia kura 2020, tumuachie tu atuongoe kwa miaka mingine 30.
 
Ukimuangalia vizuri....utaona kama anatetemeka flani hivi...inshort yupo uncomfortable...hii yote ni kwa sababu anatambua kua anadanganya.....
 
Dkt. Abbas amesema mapato ya serikali yameongezeka na isingekuwa na maana kama mapato ya serikali yanaongezeka alafu yanavuja, amedai kuna watu hawajamuelewa Rais Magufuli kwani sio mwanasiasa bali ni mtendaji na anachokisema ndio anachokifanya(Ana ukweli mchungu kuliko ahadi tamu).

Dkt. Abbas ameyasema hayo akiwa kwenye kipindi cha Clouds 360, pia ameongelea mapato akitolea mfano mizigo bandarini akisema imeshuka kidogo lakini mapato yameongezeka kutoka bilioni 703 ya zamani mpaka 780 mwaka huu sababu ikiwa mapato kuvuja siku za nyuma.

Kuhusu ndege kushikiliwa, amesema kisheria ndege haijakabidhiwa kwa watanzania na kuhoji wakiishikilia watashikilia ndege ya nani? Amekiri mgogoro huo uilkuwepo lakini wanasheria wameingilia kati na ikifika watawataarifa watanzania kwani ipo katika hatua za mwisho.

Kuhusu watumishi wa umma, amesema mikataba inakuja ambayo itakuwa na malengo na itawafanya watu wakumbuke majukumu yao wakijua wasipoyatimiza kuna hatua zitachukuliwa.

Kuhusu serikali itawaachaje kazi zikiboreshwa! Amesema katika serikali ya awamu ya tano waligundua kuna matatizo makubwa kwenye utumishi, amesema serikali inawajali sana na kuanzia mwezi huu, neema itaanza kuonekana.
Upuuuzi mtupu, kama siyo mwanasiasa kwenye chama cha siasa anafanyako nini, mwenyekiti wa chama cha siasa asiwe mwanasiasa!
 
huyu nae upropesa wake tabu kwlkwl haya siyo mwanasiasa viwanda vijengeni sasa
 
Dkt. Abbas amesema mapato ya serikali yameongezeka na isingekuwa na maana kama mapato ya serikali yanaongezeka alafu yanavuja, amedai kuna watu hawajamuelewa Rais Magufuli kwani sio mwanasiasa bali ni mtendaji na anachokisema ndio anachokifanya(Ana ukweli mchungu kuliko ahadi tamu).

Dkt. Abbas ameyasema hayo akiwa kwenye kipindi cha Clouds 360, pia ameongelea mapato akitolea mfano mizigo bandarini akisema imeshuka kidogo lakini mapato yameongezeka kutoka bilioni 703 ya zamani mpaka 780 mwaka huu sababu ikiwa mapato kuvuja siku za nyuma.

Kuhusu ndege kushikiliwa, amesema kisheria ndege haijakabidhiwa kwa watanzania na kuhoji wakiishikilia watashikilia ndege ya nani? Amekiri mgogoro huo uilkuwepo lakini wanasheria wameingilia kati na ikifika watawataarifa watanzania kwani ipo katika hatua za mwisho.

Kuhusu watumishi wa umma, amesema mikataba inakuja ambayo itakuwa na malengo na itawafanya watu wakumbuke majukumu yao wakijua wasipoyatimiza kuna hatua zitachukuliwa.

Kuhusu serikali itawaachaje kazi zikiboreshwa! Amesema katika serikali ya awamu ya tano waligundua kuna matatizo makubwa kwenye utumishi, amesema serikali inawajali sana na kuanzia mwezi huu, neema itaanza kuonekana.

Amesema uhakiki wa madeni umefanyika na nusu ya madeni yaliyopolekwa serikali yameonekana hayastahiki kulipwa, amewataka wazabuni wote wanaoidai serikali wawasilishe uthibitisho na madeni hayo yatalipwa. Amesema utaratibu wa sasa, sio kupeleka madeni jumla(Lumpsum) bali taasisi au wizara ikiwasilisha madeni isime pia nani anawadai na kwa ajili ya nini.

Kuhusu deni la taifa, amesema kwa kawaida mtu anakopa kwa sababu ana uwezo wa kulipa hivyo tunakopesheka, amesema nchi zote duniani zina madeni, amesema mtu anakopa kwa sababu kitu unachotaka kufanya kwa leo, fedha huna ila utazipata.

Amesema kukopa ni kawaida sana, amesema serikali ni tajiri na watu wasibabaike kwani tupo ndani ya kiwango tunachoruhusiwa kukopa.
Msemaji umemtukana Rais wa Tanzania. Ni sawa na kusema kawatia aibu kisiasa na mnahaha kumkwepesha na siasa. Mlitaka asifiwe kisiasa lakini imeshindikana kwa kuwa hafundishiki. Hata hivyo ni muhimu kufahamu kwamba Rais wenu ni mwanasiasa tena aliyebobea katika falsafa za kidikteta. Ni mwanasiasa dikteta, so kusema siyo mwanasiasa ni kumtukana na ingestahili awachukulie hatua kali za kinidhamu.
 
Si mwana siasa maana ccm ni taasisi ya .....Na hata linapotajwa jina ccm huwa haimaanishwi kuwa ni chama cha siasa.Pia mfumo hivi siasa umebadilishwa,si lazima kiongozi atokane na chama cha siasa.
 
Hapo patamu ,KANISANI KAINGIA GOLO.
RAISI KAWA RAHISI HIVI?
Eti mchapa Kazi,ivi si tumemchagua ili yeye awe kiongozi sisi ndo tufanyekazi?
Wasaidizi wake wanampotosha
 
Kweli
Salim+Amin+20171002_102711.jpg
 
Nimefurahi kumuona Dr Abas ambaye ni msemaji wa serikali akiwa kwenye hali ya utulivu na weledi mkubwa.

Nimependa zaidi alivyosema kuwa mojawapo ya Changamoto inayoikabili jamii yetu ni "Mshutuko wa mabadiliko"

Hakuna aliyedhania kuwa mabadiliko ya utendaji wa Serikali yangeweza kugusa sekta zote hadi nje ya mipaka yetu.

Hongera na pongezi nyingi kwako Dr Abbas.
 
Ccm sio chama cha siasa nimegundua leo, mana mwenyekiti wake sio mwanasiasa. Big up sana msemaji wetu
 
Nimeipenda hii "Amesema mshtuko upo kwa baadhi ya watu ambao pesa kwao imepotea lakini changamoto ya mshtuko ipo kwa nchi zote ambazo zilitaka kupiga hatua, amesisitiza pesa wanazopata serikali hawatumii wao bali zinarudishwa kwa wananchi"
NA hii "Kuhusu ndege kushikiliwa, amesema kisheria ndege haijakabidhiwa kwa watanzania na kuhoji wakiishikilia watashikilia ndege ya nani? Amekiri mgogoro huo ulikuwepo lakini wanasheria wameingilia kati na ikifika watawataarifa watanzania kwani ipo katika hatua za mwisho".
 
Back
Top Bottom